Tarehe : Feb. 28, 2023, 8:19 a.m.
Awaahidi Ushirikiano, akaribisha mazungumzo yenye kujenga Sekta
Rais Samia amteua Mhandisi Samamba kuwa Katibu Mtendaji Tume ya Madini
Naibu Waziri Dkt. Kiruswa apongeza Uteuzi wake
Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake leo Februari 27, 2023, wamempokea Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Madini Kheri Mahimbali katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu.
Akizungumza na watumishi katika kikao kifupi baada ya kuwasili ofisini hapo, Mahimbali ameomba ushirikiano ili kuijenga sekta ya Madini na kueleza kuwa, mlango uko wazi kwa mazungumzo yatakayoongeza tija kwenye sekta.
" Mimi si mbobezi kwenye masuala ya madini lakini ninategemea kujifunza mengi kutoka kwenu na hivyo ninawaahidi ushirikiano tufanye kazi kama timu moja," amesema Mahimbali.
Awali, akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amemweleza Katibu Mkuu Mahimbali kuwa viongozi na watumishi wa wizara wako tayari kushirikiana naye kwa dhati kwa maendeleo ya sekta ya madini.
Katika hatua nyingine, Dkt. Kiruswa amepongeza uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba ambaye ameteuliwa na Rais Samia wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
" Katibu Mkuu, Samamba ni moja ya watendaji tunaovutiwa naye," amesema Dkt. Kiruswa.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.