[Latest Updates]: Waziri Mavunde Aainisha Mikakati ya Kumaliza Migogoro Mirerani

Tarehe : April 7, 2024, 10:05 p.m.
left

-Serikali yarusha ndege ya Utafiti ndani na nje ya ukuta kupata kupata viashiria vya mwamba wa madini

-Taarifa za utafiti kusaidia kuwaongoza vizuri wachimbaji

-Atoa tuzo kwa wachimbaji wanaorudisha kwa jamii(CSR)

-Aongoza futari ya pamoja na wachimbaji wadogo

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema serikali itahakikisha inakuja na suluhisho la migogoro baina ya wachimbaji inayojitokeza katika eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite ili kuchochea uzalishaji zaidi wa madini hayo ya vito.

Hayo yamesemwa leo Mirerani,Manyara na Waziri Mavunde wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa Wachimbaji waliotekeleza mpango wa wajibu kwa jamii (CSR) kwa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro,Mkoani Manyara.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan imerusha ndege nyuki ndani na nje ya ukuta wa Mirerani kubaini viashiria vya mwamba wa madini  hatua ambayo itapelekea wachimbaji wengi kuchimba kwa uhakika.

Kupitia utaratibu huu wa kupata viashiria vya mwamba wa madini itasaidia kutatua changamoto ya mtobozano chini ya ardhi kwa wachimbaji wengi kujikuta eneo moja  la uchimbaji na hivyo kupelekea migogoro miongoni mwao.

Ninawapongeza wachimbaji wote mliorudisha kwa jamii kwa kuboresha huduma za Afya na Elimu,niwaombe Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na Chama cha Wachimbaji Manyara(MAREMA)kuweka utaratibu mzuri zaidi ili kundi kubwa la wachimbaji liweze kuchangia huduma za msingi kwa jamii”Alisema Mavunde

Akitoa salamu zake,Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka ameishukuru Serikali kwa kuendelea na ujenzi wa kituo cha Biashara ya Madini-Tanzanite Exchange Centre(TEC) ambacho kitachochea maendeleo na ukuaji wa kasi wa Mji wa Mirerani.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Queen Sendiga amewataka wamiliki wa Leseni kuwa mstari wa mbele kuchochea maendeleo ya Jamii zinazonguka machimbo ya madini ili kuboresha huduma za msingi na kukuza uchumi wa Jamii husika.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals