Tarehe : June 28, 2018, 4:22 a.m.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Prof. Shukran Manya leo tarehe 28 Juni, 2018, amepokea ripoti ya Ukaguzi Maalum wa Migodi ya Madini ya Vito na Madini ya Kinywe (Graphite) kutoka kwa Mwenyekiti wa Timu ya Ukaguzi Profesa Justinian Ikingura.
Mwenyekiti wa Timu Maalumu ya Ukaguzi wa Migodi ya Vito na Madini ya Kinywe (Graphite) Profesa Justinian Ikingura akikabidhi Ripoti ya Ukaguzi huo kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Profesa Shukrani Manya, makabidhiano haya yamefanyika tarehe 28/6/2018 katika ukumbi wa mikutano wa GST. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula na Profesa Abdukarim Mruma pamoja na watalam wa timu hiyo
Ripoti hiyo imetokana na Tume Maalum ya Wataalam Sita iliyoundwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Prof. Manya tarehe 17 Juni, 2018 ikilenga kufanya ukaguzi maalum katika maeneo ya uchimbaji wa madini ya Vito na Kinywe katika wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro.
Aidha, ukaguzi huo ulilenga kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko aliyoyatoa hivi karibuni wakati wa ziara yake mkoani Morogoro.
Katika ziara ya Naibu Waziri Biteko mkoani humo, alipokea malalamiko kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini ya vito ambao ni wanakijiji wa kijiji cha Epanko kilichopo katika eneo la mradi wa madini hayo.
Aidha, kufuatia malalamiko hayo Naibu Waziri aliahidi kuunda timu ya watalaam wa madini itakayofanya kazi ya ukaguzi maalum kwa lengo la kutathmin uendeshwaji wa migodi ya madini ya vito na kinywe pamoja na biashara ya madini kulingana na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 pamoja na marekebisho yake.
Katika ripoti hiyo, timu ya wataalam wa madini imetoa mapendekezo mbalimbali ikiwemo Serikali kupitia Wizara ya Madini na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kuweka mkakati wa kufanya Utafiti na tathmin ya madini adimu ya vito katika eneo la Mahenge na maeneo mengine nchini ili kuwepo na takwimu sahihi za kuvutia wawekezaji katika uchimbaji wa madini hayo.
Pendekezo jingine ni Mamlaka husika kuweka mpango wa kutoa huduma ya uthaminishaji wa madini ya vito katika maeneo ya wachimbaji wadogo ili kuwezesha wachimbaji hao kupata bei stahiki ya madini wanayozalisha na hivyo kuongeza kipato chao na kulipa tozo stahiki kwa Serikali.
Wajumbe wa timu hiyo walitoka katika Taasisi ya Jiolojia ya Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Chuo cha Madini Dodoma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Ukaguzi wa Migodi na Afisa Madini Mkazi wa Dodoma.
Na Samwel Mtuwa, Dodoma
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.