Tarehe : May 18, 2018, 10:46 a.m.
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia ya Afrika, Taasisi ya Kijiolojia ya Ulaya, Umoja wa Ulaya pamoja na Muungano wa Afrika na Ulaya katika tasnia ya Jiosayansi wametoa mafunzo juu ya Urithi wa Kijiolojia (Geoheritage) kwa Mwaka 2018.
Waratibu na Wasimamizi wa Mafunzo yenye lengo la kuongeza uelewa na ujuzi katika Sekta ya jiosayans na vivutio vya kijiolojia iliyoendeshwa na GST kwa ushirikiano wa PanAfGeo na Umoja wa Ulaya. Wa kwanza kutoka kushoto ni Joshua Mwankunda kutoka NCAA, anayefuata ni John Kalimenze kutoka GST, Enriqu Diaz kutoka IGME.[/caption]
Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Jiolojia kutoka GST Maruvuko Msechu alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha na kuongeza ufahamu pamoja na ujuzi juu ya sekta ya madini barani Afrika hususani katika taasisi za jiolojia Afrika pamoja na kuvumbua vivutio vingi vya utalii wa kijiolojia kupitia urithi wa kijiolojia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Jiolojia kutoka GTS John Kalimenze, alisema lengo kuu la mafunzo hayo ilikuwa ni kupeana ujuzi na kuongeza uelewa kupitia uwasilishaji wa mada mbalimbali kama vile mafunzo juu ya upimaji wa ramani za jiosayansi, uchunguzi juu ya rasilimali madini, uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo na usimamizi wa mazingira katika uchimbaji madini.
Mmoja wa Waratibu na Msimamizi wa mafunzo hayo kutoka nchini Hispania Enriq Diaz alitoa mada juu ya utunzaji wa uzuiaji wa uchimbaji holela wa madini kwa lengo la kuonyesha njia bora za kutunza urithi wa vivutio vya kijiolojia duniani.
Mafunzo hayo yanayofanyika kila mwaka yalianza tarehe 14- 19 Mei, 2018 na kushirikisha washiriki kutoka nchi mbalimbali kutoka barani Afrika zikiwemo Liberia, Botswan, Sudani ya kaskazini, Nigeria, Commoro, Moroco, Zimbambwe, Namibia.
Na Samwel Mtuwa, GST
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.