[Latest Updates]: Wizara ya Madini yaendesha mafunzo ya ufungaji migodi

Tarehe : March 28, 2018, 9:01 a.m.
left

Wizara ya Madini kupitia Kitengo cha Mazingira kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa kutoka nchini Canada (CIRDI) wameanza kutoa mafunzo ya ufungaji wa migodi  kwa wataalam kutoka Taasisi za Serikali zinazosimamia Sekta ya Madini ndani na nje ya nchi.

Wataalam wa Madini kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa katika mafunzo ya ufungaji migodi yaliyoratibiwa na Wizara ya Madini na Taasisi ya Kimataifa kutoka nchini Canada (CIRDI).[/caption]

Mkuu wa Kitengo cha Mazingira katika Wizara ya Madini,   Gidion  Kasege amesema kuwa wataalam hao watapata mafunzo kuhusu ukokotoaji wa mahesabu ya gharama za ufungaji migodi, usimamizi wa maji migodini na jinsi ya kutengeneza sehemu ya kuhifadhia mabaki ya uchenjuaji (mining tailings).

Alisema kuwa, hii ni mara ya pili kwa Taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa wataalam hao wa Madini na kwamba Awamu hii imeshiriksha nchi nyingine za Afrika ili wataalam hao waweze kubadilishana uzoefu na kujifunza mafanikio na changamoto ambazo nchi hizo zinapata katika shughuli za ufungaji wa migodi.

Alieleza kuwa nchi zinazohudhuria mafunzo hayo ni Tanzania, Kenya, Namibia na Ethiopia, ambapo mafunzo yanatolewa kwa njia ya nadharia na vitendo katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita  (GGM) na Buzwagi uliopo mkoani Shinyanga.

Naye, Afisa katika Ofisi ya Madini mkoani Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumburu ameeleza kuwa kupitia mafunzo hayo wataalam wataongeza uelewa katika shughuli za usimamizi wa migodi nchini na hivyo kuhakikisha kuwa migodi inafuata taratibu zote zinazotakiwa wakati wa usitishaji wa shughuli zao nchini.

Alisema kuwa kupitia changamoto ambazo nchi nyingine wamepata katika shughuli hizo za madini,  itawasaidia kuwa makini zaidi wa utekelezaji wa shughuli hizo nchini.

Wataalam wa Madini kutoka Tanzania na Ethiopia wakifuatilia mafunzo ya ufungaji migodi yaliyokuwa yanatolewa na wakufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya nchini Canada (CIRDI).[/caption]

Kwa upande wake, Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Madini, Innocent Makomba, alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa wataalam kwani yanaongeza uelewa wa masuala yanayopaswa kutekelezwa kabla ya ufungaji wa migodi ikiwemo suala la kushirikisha jamii inayozunguka migodi kabla ya kufanyika kwa maamuzi.

" Tunajifunza kuwa ni muhimu kushirikisha jamii kwani  wao wanaweza kuamua kuwa maeneo ambayo uchimbaji umeshafanyika yatengenezwe kwa ajili ya kufanyia shughuli nyingine kama uvuvi, kilimo au hata kuwa makazi ya watu na kupitia mafunzo haya tumeona mifano ya jinsi nchi nyingine zilivyotekeleza suala hilo," alisema Makomba.

Vilevile, Makomba alisema kuwa mafunzo hayo yamewaongezea uelewa katika suala utengenezaji wa sehemu za kuhifadhia mabaki ya uchenjuaji (mining tailings) ili zisilete madhara kwa wananchi au mazingira.

Imeandaliwa na:

Teresia Mhagama,

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals