[Latest Updates]: Katibu Mkuu Mahimbali Akamilisha Ziara ya Siku Mbili Wilayani Chunya

Tarehe : June 10, 2024, 10:37 p.m.
left

● Atembelea migodi midogo ya uzalishaji na uchenjuaji dhahabu.

●Apokea changamoto za wachimbaji wadogo.

Chunya 

Katibu Mkuu Wizara ya Madini,Kheri Mahimbali  Juni 9, 2024 amekamilisha ziara yake katika mkoa wa kimadini  kwa kutembelea migodi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu wilayani chunya,Mkoa wa Mbeya.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Mahimbali amekamilisha kwa kutembelea migodi mbalimbali ya uchimbaji pamoja na kuona jinsi  uchenjuaji wa madini ya  dhahabu unavyofanyika katika eneo la Makongolosi na Itumbi.

Sambamba na ziara hiyo, Mahimbali amepokea Taarifa ya Uchimbaji na Uchenjuaji wa Madini ya Dhahabu pamoja na Hali  ya Ushirikishwaji wa Jamii kutoka katika kampuni ya  Apex Resources Ltd na Xepa Resources Ltd zinazojishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Itumbi wilayani Chunya.

Katika ziara hiyo, Mahimbali amepata fursa ya  kuzungumza na wachimbaji wadogo katika eneo la Itumbi na kupokea changamoto mbalimbali zinazowakabili katika shughuli zao za uchimbaji madini.

Ziara hiyo maalum yenye lengo la kutembelea maeneo mbalimbali ya uchimbaji na uchenjuaji imejumuhisha watendaji  kutoka Wizara ya Madini na Taasisi zake.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals