[Latest Updates]: Dkt. Biteko asisitiza wadau kushiriki Kongamano Uwekezaji Skkta ya Madini 2023

Tarehe : June 5, 2023, 8:30 a.m.
left

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa wadau wote wa madini wa ndani na nje ya nchi kushiriki katika Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini linalotarajiwa kufanyika Oktoba 25 na 26, 2023.

Ametoa wito huo katika hafla fupi iliyozikutanisha Kampuni mbalimbali zilizowekeza nchini hususan katika Sekta ya Madini iliyo fanyika Juni 02, 2023 jijini Dar es Salaam.  

Aidha, Dkt. Biteko amesema Australia ni Taifa la mfano na lenye kupaswa kuigwa katika uwekezaji wa Sekta ya Madini ambalo lina uzoefu mkubwa katika shughuli za uwekezaji wa madini.

“Hivi karibuni Taifa limeshuhudia utiaji saini mikataba ya uchimbaji mkubwa na wa kati wa madini muhimu ya Kinywe na Rare earth element wenye thamani za dola za Marekani Milioni 667 kwa  Kampuni tatu  kutoka nchini Australia,” amesema Dkt. Biteko. 

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Biteko amesema lengo la Tanzania ni kutoa mchango mkubwa  katika mnyororo mzima wa upatikanaji wa madini muhimu ulimwenguni kwa lengo la kuiokoa dunia katika mabadiliko ya hali ya hewa.

Pia, amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Australia katika nyanja mbalimbali hususan katika uchimbaji na uchenjuaji wa madini ili kuongeza tija katika sekta hiyo.

Sambamba na hayo, Dkt. Biteko amesema Serikali itaendelea kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wadau wa Sekta ya Madini ili kuiwezesha sekta hiyo kuchangia asilimia 10 ya Pato la Taifa ifikapo Mwaka 2025 ambapo mpaka sasa mchango wa sekta hiyo kwenye Pato la Taifa umeongezeka na kufikia asilimia 9.7.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals