[Latest Updates]: Maendeleo Uwekezaji Mradi wa Liganga na Mchuchuma

Tarehe : Nov. 14, 2024, 4:27 p.m.
left

●Utazalisha tani 219 za Chuma.

●Tani 175,400 za Titanium

●Tani 5000 za Vanadium

Tanzania

Wakati Serikali ikiendelea na  jitihada mbalimbali za  kutafuta mwekezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma uliopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,Tanzania inatarajiwa kuwa mzalishaji mkubwa wa madini ya chuma Barani Afrika.

Wakati jitihada hizo zikiendelea mnamo  Agosti 3 , 2024  Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) lilitia saini makubaliano ya uchimbaji wa makaa ya mawe na chuma katika mradi wa Maganga Matitu na kampuni ya Fujian Hexingwang Industry Tanzania Co.Ltd  itakayowekeza kiasi cha Dola za Marekani milioni 77.

Ikumbukwe kwamba hivi karibuni ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania , Dkt.Samia Suluhu Hassan aliiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara , Mipango na Uwekezaji  kukamilisha mchakato wa kupata kampuni itakayowezesha kuanza kwa mradi wa Liganga na Mchuchuma.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa mradi wa Liganga na Mchuchuma ukikamilika utazalisha kiasi cha  tani milioni 219 za chuma ambazo zitadumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 70, na madini mengine yatakayotokana na mgodi huo ni pamoja na Titanium tani 175,400 kwa mwaka na madini aina ya Vanadium tani 5000 kwa mwaka.

Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa msongo wa umeme wa kilovoti 220 , uanzishwaji wa kiwanda cha kuchenjua chuma na bidhaa zitokanazo na chuma.

#TanzaniaMiningIvestment
#MiningValueAddition
#InvestInTanzania

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals