[Latest Updates]: Waziri Mavunde Avutiwa na Kijiji cha Stamico Maonesho ya Madini Geita

Tarehe : Oct. 9, 2024, 6:31 p.m.
left

Waziri wa Madini,Mhe.Anthony Mavunde amevutiwa na ubunifu  wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wa kuwaweka wadau wake eneo moja kwenye  Maonesho ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Mhe.Waziri ametoa pongezi hizo leo tarehe 9 Oktoba wakati alipotembelea banda la STAMICO ambalo limepewa jina la "Kijiji cha STAMICO na Wadau Wake".

Alivutiwa  jinsi washiriki walivyojipanga kwa bidhaa mbalimbali kwenye sekta ya madini.

Pia alivutiwa na vikundi vya wanawake,watu wenye ualbino na watu wenye ulemavu wa usikivu ambao wanashiki kwenye maonesho haya kwa udhamini wa STAMICO.

Mhe.Waziri aliambatana kwenye ziara hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhe.Martin Shigela pamoja na maofisa wengine kutoka serikalini.

Vikundi ambavyo vimealikwa na STAMICO na kushiriki ndani ya banda moja ni pamoja na FEMATA,TAWOMA, TAMAVITA,FDH,Tanzania Youth Miners na Chama cha Wachimbaji Geita (GEREMA).

Wengine ni pamoja na kikundi cha Wanawake na Samia Geita na Chama cha Wanawake Geita (GEWOMA

Mhe.Waziri amepokelewa na Kaimu Meneja wa Masoko na Mahusiano wa STAMICO,Bw Gabriel Nderumaki ambae alimpatia maelezo mafupi kuhusu ushiriki wa Shirika kwenye maonesho haya mwaka huu. 

Bw Nderumaki amesema kuwa STAMICO inajivunia kufanya kazi na vikundi mbalimbali vya wachimbaji na kuongeza  kuwa Shirika litaendelea kuvilea hivi vikundi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals