[Latest Updates]: Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa Avutiwa na Mkakati wa Serikali wa Utafiti wa Madini Nchini

Tarehe : Jan. 27, 2025, 1:08 p.m.
left

▪Ampongeza Rais Samia kwa kwa maono ya kukuza sekta ya Madini

▪Avutiwa na aonesha utayari wa kusaidia VISION 2030 

▪Apongeza mpango wa serikali wa kuongeza thamani madini mkakati nadani ya nchi

Dar es salaam

Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Mhe. Amina  Mohamed ameipongeza serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mkakati wa kufanya utafiti wa kina wa kijiolojia na utafutaji madini nchini.

Naibu Katibu Mkuu Amina Mohamed ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa pembeni wa Mkutano wa Nishati alipokutana na Waziri wa Madini Mhe Anthony Mavunde.

“Naipongeza Tanzania chini ya uongozi wa Mhe. Rais Samia ambao umekuja na ubunifu mkubwa katika maeneo mbalimbali.

Mpango wa kufanya utafiti wa kina kupitia Vision2030 ni mpango ambao tunauunga mkono kwa kuwa una lengo la kubaini madini ambayo mnayo na hivyo kujiapanga vyema juu ya uvunaji wa madini hayo.

Dunia hivi sasa ina mahitaji makubwa ya madini mkakati,Tanzania imebarikiwa kuwa na madini hayo kwa uwingi hivyo suala la uongezaji thamani,utunzaji wa mazingira na kulinda jamii zinazoishi katika maeneo ya uchimbaji wa madini ni vyema yakazingatiwa wakati wa uandaaji wa mkakati maalum wa uvunaji wa madini ya kimkakati.

Umoja wa Mataifa kupitia programu zake mbalimbali za utunzaji wa mazingira ipo tayari kuunga mkono jitihada hii kubwa ya serikali ya Tanzania“amesema Mhe. Mohamed.

Akizungumza katika mkutano huo,Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kipaumbele cha sekta ya Madini kwa hivi sasa ni kufanya utafati wa kina ili kuiwezesha nchi kupata taarifa za kiwango na ubora wa madini iliyonayo.

Amongeza kwamba, utafiti wa kina utaleta matokeo chanya kwenye maeneo ya kijamii na kiuchumi na hivyo kusaidia kuchochea maendeleo ya Tanzania,kwakuwa pamoja na mafanikio yote ya kwenye sekta ya madini eneo ambalo limefanyiwa utafiti ni asilimia 16% ya eneo la nchi nzima.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals