[Latest News]: Naibu Waziri wa Madini Dkt. Kiruswa Aielekeza GST Kufanya Utafiti wa Madini Longido

Tarehe : June 6, 2022, 3:26 a.m.
left

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST)  inatakiwa kufanya utafiti  ili kujua aina za madini  yaliyopo katika maeneo yenye shughuli za uchimbaji mdogo wa madini wilaya ya Longido.

Wito huo, umetolewa leo Juni 4, 2022 na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa wakati akifunga semina ya Siku Mbili iliyotolewa kwa wazee wa mila na wataalam wa Wizara ya Madini iliyolenga kuelimisha masuala mbalimbali yanayohusu Sheria ya Madini, Uchimbaji,  Usimamizi wa Mazingira na Wajibu wa migodi kwa jamii katika maeneo ya uchimbaji wilayani Longido mkoa wa Arusha.

Dkt. Kiruswa amesema  hayo baada ya kupokea maoni kutoka kwa wazee wa mila, wadau, wafanyabishara na wachimbaji wadogo wa madini kuwa wanachimba kwa kubahatisha.

Amesema, GST imetakiwa ifanye utafiti wa kutosha katika wilaya ya Longido hususan katika eneo la Matale yanapochimbwa madini ya Ulanga ili kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha. Amesisitiza kuwa, wanakosa taarifa za kijiolojia ya maeneo hayo ili wachimbe kwa tija.

"Baada ya wao kuwa wamepata elimu na wanajua taratibu zilizopo, ninatoa wito kwa GST wafanye haraka na wafike kufanya utafiti ili kujua kuna aina gani ya madini na ikiwezekana watengeneze ramani ili wananchi waone maeneo yenye rasilimali madini," amesisitiza.

Pia,  semina hiyo imesaidia kutoa uelewa mpana wa shughuli zinazofanyika katika Sekta ya Madini katika masuala ya Sheria, Leseni, Utafiti, Ushirikishwaji wa Watanzania na Wajibu wa Makampuni kwa jamii zinazozunguka migodi.

Vile vile, amesema kuwa elimu hiyo waliyoipata  ni hatua muhimu ambayo itasaidia kutekeleza shughuli za madini kwa wale wanaohitaji kuwekeza na ambao wamepata elimu ya  namna gani wanaweza kuomba leseni za uchimbaji, uongezaji thamani madini ya Vito na kusafirisha kwenye masoko ya madini ndani na nje ya nchi na biashara ya madini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Longido Nurdin Babu, amewataka wazee wa mila na wadau wa Sekta ya Madini kujitokeza kuwekeza katika biashara ya madini ili kutumia elimu waliyoipata katika mafunzo baada ya kuelimishwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Madini.

Semina imetolewa katika wilaya ya Longido na wataalam wa Wizara ya Madini imelenga kuelimisha fursa zilizopo katika Sekta ya Madini, Kanuni na Miongozo mbalimbali ya Taasisi za wizara na Sheria ya Madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals