[Latest Updates]: Waziri Mkuu Majaliwa Azindua Mifumo ya Kidigitali Katika Utumishi wa Umma

Tarehe : June 23, 2024, 2:58 p.m.
left

Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  amezindua Mifumo ya kidigitali ya Uwajibikaji na Usimamizi ya Utendaji katika Utumishi wa Umma ambayo imejengwa na watumishi wa ndani kutoka taasisi mbalimbali za umma na inasimamiwa na Serikali kwa asilimia 100.

Waziri Mkuu Majaliwa amezindua mifumo hiyo leo Juni 23, 2024 katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika kuanzia tarehe 16- 23, Juni, 2024 katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesisitiza kuhusu taasisi za umma kuweka Mipango madhubuti ya kutumia mifumo ya kiditali ili kuleta mapinduzi katika utendaji kazi ikiwemo kurahisisha shughuli za utoaji huduma kwa umma.

Maadhimisho ya Mwaka huu yamehusisha baadhi ya taasisi za umma ikiwemo Wizara ya Madini.

Wizara ya Madini ilitumia fursa hiyo kuelimisha Wananchi na Watumishi waliotembelea banda kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini ambapo pia, wananchi wakitumia nafasi hiyo kutoa maoni yao.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa umma huadhimishwa kila mwaka katika tarehe tajwa ambapo mwaka 2024 yameongozwa na Kaulimbiu isemayo  Kuwezesha kwa Utumishi wa Umma uliojikita kwa Umma wa Afrika ya karne ya 21 iliyojumuishi na inayostawi; Ni safari ya mifumo na mabadiliko ya teknolojia,"

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals