[Latest Updates]: Mradi wa Madini Tembo Utaiweka Tanzania katika Ramani ya Dunia - Waziri Mavunde

Tarehe : Feb. 21, 2024, 11:56 a.m.
left

Utakuwa Mradi wa kwanza kuwa na Leseni Kubwa ya Uchimbaji Madini mkoani Tanga

Mradi kutoa kwa ajira zaidi ya watu 1,000

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa Mradi Mkubwa wa Uchimbaji Madini Tembo unaotarajiwa kutekelezwa wilayani Pangani Mkoa wa Tanga utaiweka Wilaya hio pamoja na Tanzania kwa ujumla katika ramani ya dunia.

Ameyasema hayo Februari 20, 2024 alipotembelea eneo la Tajiri lililopo wilayani  humo ambako Mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa na Kampuni ya Nyati Mineral Sands Limited yenye ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Strandline Resources Limited kutoka nchini Australia mara baada ya utaratibu wa upatikanaji leseni kukamilika.

Waziri Mavunde amesema kuwa Mradi huo utasaidia kutangaza fursa zilizopo nchini za madini hayo duniani pamoja kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi nchini pamoja na pato la mtu mmoja mmoja kwa kutoa nafasi za ajira kwa wananchi na wenyeji wa Pangani.

“Kwa mujibu wa Sheria ya Madini, leseni kubwa ya uchimbaji wa madini [Special Mining License – SML] inatolewa na Baraza la Mawaziri kwahiyo tunasubiri vikao vya Baraza la Mawaziri kwakuwa tumeshakamilisha taratibu kwa kushirikisha taasisi mbalimbali zinazohusika pamoja na wananchi wenyeji wa Pangani ambao wameonyesha kuwa wameukubali na wanautaka mradi” amesema Mhe. Mavunde. 

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni matunda ya mazingira mazuri yanayovyutia uwekezaji yaliyowekwa hapa nchini na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwamba itasaidia ukuaji na mchango wa sekta kwenye Pato la Taifa. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya Pangani Zainab Abdallah amesema kuwa Mradi huo wa kwanza kuwa na leseni kubwa ya uchimbaji wa madini mkoani Tanga utasaidia kufungua fursa za ajira kwa wakazi wa wilaya hiyo kupitia ushirikishwaji wa Watanzania katika mradi (Local Content) pamoja na wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR) huku akikaribisha wawekezaji wengine kwenda kuwekeza katika wilaya hiyo. 

Naye, Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyati Mineral Sands Limited kwa upande wa Serikali, Mhandisi Heri Gombera amesema kuwa Mradi huo unatarajiwa Tani milioni 8 kwa mwaka ya Madini Tembo na kutokana na utafiti wa sasa unaonyesha kuwa uhai wa mgodi huo ni kati ya miaka 20 hadi 25 ambapo katika kipindi hicho makusanyo ya Serikali yanakadiriwa kufikia dola za Marekani milioni 457.24 sawa na shilingi trilioni 1.145.

Madini hayo hutumika katika mitambo ya nyuklia pamoja na kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mapambo, vifaa tiba, injini za ndege, saa, simu, kompyuta mpakato (laptop) na vyungu vya kuyeyushia metali pamoja na kutengenezea marumaru.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals