[Latest Updates]: Aliyoyasema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika Hafla ya Uapisho wa Viongozi Wateule Iliyofanyika Tarehe 5 Julai, 2024 - Zanzibar

Tarehe : July 5, 2024, 10:48 p.m.
left

Zanzibar

WIZARA YA MADINI

#Nimefurahi kukujua leo maana nilikuwa nakusikia tu hongera kwa kuwa Katibu Mkuu. Waziri yuko pale najua mtakwenda kufanya vizuri. Wewe nimekutoa Tume ya Madini maana niliambiwa umefanya kazi nzuri sana, kwa hiyo nafasi yako ya Katibu Mkuu unaijua Tume vizuri najua utaisimamia vizuri.

#STAMICO tumefanya uwekezaji mkubwa sana na wamefanya vizuri, walipata zawadi kutokana na kufanya mageuzi makubwa na hata kwenye utoaji wa gawio kwa Serikali kwa hiyo nenda ukawasimamie vizuri shirika lisonge mbele.

 #Kinachoniumiza kichwa ni kwenye leseni, mmetoa leseni nyingi watu wameshikilia lakini hakuna uwekezaji hakuna chochote kinachoendelea, nenda kalisimamie hilo. Waziri na mwenzie walishaanza kuangalia nani amefanya nini, nani ana nia na ana uhalali gani, nenda kalisimamie hilo. 

#Sasa hivi nimetoka kuzungumza na Rais wa Benki ya Uwekezaji wa Europe (Ulaya) ananiuliza vipi huko madini kuna nini? Nimemwambia tumefanya utafiti wa kina kwa asilimia 16 tu kwa nchi nzima kama mnaweza mtusaidie kwenye hilo ili tujue tuna nini kwa kiasi gani. GST iongezewe nguvu ifanye  tafiti za madini maeneo yote.

#Wachimbaji wadogo huko nyuma tulikuwa tunawaona kama kero lakini wameibeba Sekta. Juzi niliona taarifa ya kutoroshwa kwa madini ya dhahabu kutoka Afrika ya zaidi ya dola bilioni 35. Nenda kasimamie mapato ya dhahabu yarudi nchini, hatuna sababu ya kulia kwa kukosa dola.

 #Hitimisho, ninawapongeza na ninawapa pole kwa kuamininiwa, mkafanye kazi kama Sheria zinavyotaka uongozi ni dhamana.

#InvestInTanzaniMiningSector

#Vision2030:MadininiMaisha&Utajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals