[Latest Updates]: Wizara ya Madini Yakutana na Wamiliki Wakubwa wa Viwanda vya Kusafisha Dhahabu Nchini

Tarehe : May 28, 2024, 12:50 p.m.
left

Dodoma

Wizara ya Madini leo  Mei 28, 2024 imekutana na wamiliki wakubwa wa viwanda vya kusafisha madini ya dhahabu nchini kwa lengo la kujadili namna ya kutatua  changamoto zilizopo na kuboresha mazingira katika mnyororo mzima wa kusafisha madini ya dhahabu.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amesema kuwa Wizara ya madini inatambua mchango wa viwanda vya kusafisha dhahabu nchini hivyo ili kuifanya sekta hii kuwa endelevu na yenye kuleta tija kwa wadau ni vyema kwa pamoja tukae na kujadiliana juu changamoto zilizopo na kuangalia namna ya kuzitatua kwa ushirikiano wa pamoja.

Mbibo ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha madini ya dhahabu yanaongezewa thamani nchini kupitia viwanda vya ndani hivyo Serikali itaendelea  kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kwa kuboresha miundombinu yote inayohusiana na sekta ya madini.

Awali, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu kufungua kikao,  Kamishna wa Madini Dkt.AbdulRahman Mwanga ameeleza kuwa ajenda kubwa ni kujadiliana juu ya masuala yanayohusiana na mazingira yote  usafishaji wa  dhahabu kuanzia ukusanyaji, ununuzi na usafirishaji.

Kwa upande wake,  Meneja Mkuu kiwanda cha kusafisha Dhahabu cha Mwanza (MPMR) Amin Tahir, amesema changamoto kubwa ni kutopatikana kwa malighafi ya kutosha kulisha kiwanda.

Tahir ameiomba Serikali kutunga sheria itakayowezesha madini ghafi ya dhahabu kusafishwa ndani ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani.

Naye, Mmiliki wa kiwanda cha kusafisha Dhahabu cha Geita (GGR) Sarah Masasi ameiomba serikali kupitia Wizara ya Madini kuweka mazingira yatakayowezesha  dhahabu inayopatikana  kutoka kwa wachimbaji wadogo na wa kati kusafishwa  ndani ya nchi.

Kikao hicho kimejumuhisha wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals