[Latest Updates]: Mwenyekiti wa Tume ya Madini akutana na Balozi wa India nchini

Tarehe : Sept. 6, 2018, 7:43 a.m.
left

Na Greyson Mwase, Dodoma

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula leo tarehe 13 Septemba, 2018 amekutana na Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya jijini Dodoma. Lengo la ziara ya Balozi Arya kwenye Ofisi ya Mwenyekiti wa Tume ya Madini lilikuwa ni kujitambulisha pamoja na kufahamu majukumu ya Tume.

Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula zilizopo jijini Dodoma[/caption]

Akizungumza katika kikao hicho, Profesa Kikula alieleza kuwa Tume ya Madini imejipanga kusimamia Sheria ya Madini ya Mwaka 2017 na  kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya madini nchini

Alisema Sheria ya Madini ina  matakwa yake kama vile  local content, utoaji wa huduma kwa jamii kwenye shughuli za uchimbaji madini (corporate social responsibility) na kiapo cha uadilifu kwenye shughuli za uchimbaji madini (integrity pledge)

Alisema kuwa Tume imejipanga pia kutoa leseni haraka iwezekanavyo na kuwasaidia wachimbaji wadogo.

Akizungumzia namna Tume ya Madini ilivyojipanga katika kutatua changamoto ya migogoro kwenye Sekta ya Madini Nchini, Profesa Kikula alisema kuwa Tume inaandaa mpango  wa kutatua migogoro kuanzia katika ngazi ya kijiji, kata, wilaya na taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa migogoro mingi inatatulika katika mamlaka za Vijiji, Kata na Wilaya. Aidha, Profesa Kikula alimwomba Balozi wa India kuendelea kutoa ufadhili kwa wataalam wa Tume ya Madini hususan  katika maeneo ya Uchimbaji wa Madini kwa kutumia teknolojia ya kisasa, Usimamizi wa Rasilimali Watu na maeneo  mengine ili  kukuza Sekta ya Madini Nchini.

“ Lengo letu ni kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi, na kama Tume  kwa kushirikiana na  Wizara ya Madini tumejipanga kuhakikisha tunakuwa na wataalam wenye weledi kwenye usimamizi  wa Sekta ya Madini. Hivyo basi mafunzo  kwa wataalam  tunayapa kipaumbele sana,” alisisitiza Profesa Kikula.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akielezea majukumu ya Tume ya Madini kwa Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya (hayupo pichani)[/caption]

Katika hatua nyingine, Profesa Kikula alimwomba Balozi wa India kuendelea kutangaza Sekta ya Madini Nchini na kusisitiza kuwa Tanzania ina maeneo mengi yenye madini yaliyofanyiwa utafiti na Taasisi ya Jiolojia na  Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

Alisisitiza kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali.

Wakati huo huo Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya alisema kuwa nchi ya India ipo  tayari kushirikiana na  Tume ya Madini hususan  katika Sekta ya Madini na kusisitiza kuwa wapo tayari kutoa ufadhili kwa watumishi wa Tume.

Aliendelea kusema kuwa nchi ya India imekuwa ikitoa mafunzo ya muda mrefu  hususan katika ngazi za Shahada za Uzamili na za Uzamivu katika vyuo bora na kusisitiza kuwa itaendelea na mpango wake wa kutoa mafunzo hususan kwenye masuala ya madini.

Katika hatua nyingine,  Balozi Arya alimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula kwa kuteuliwa kuongoza Tume hiyo pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Tume ya Madini kwenye uboreshaji wa Sekta ya Madini Nchini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals