[Latest Updates]: Biteko - Sijaridhika ushirikishwaji Wananchi Migodini

Tarehe : Sept. 17, 2019, 6:29 a.m.
left

Na Issa Mtuwa - Geita

Pamoja na kuupongeza Mgodi wa Dhahabu wa Geita  (GGM) katika masuala ya ulipaji kodi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii (CSR) na kuwa mgodi namba moja nchini kwa utekelezaji wa Sheria za Madini, bado serikali hairidhishwi na namna mgodi huo na mingine inavyowashirikisha wananchi moja kwa moja.

Kauli hiyo ilitolewa Septemba 16 na Waziri wa Madini Doto Biteko mjini Geita   kwenye mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara  na watoa huduma mbalimbali  mkoani Geita , wananchi na uongozi wa GGM. Mkutano huo uliokuwa na lengo la kufahamishana fursa za kibiashara na utoaji huduma  zilizopo kwenye mgodi wa GGM.

 “Naomba niwe mkweli, mgodi wa GGM ni wakwanza hapa nchini katika ulipaji wa kodi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii (CSR) lakini sijaridhishwa na namna ambavyo mgodi unavyo washirikisha wananchi moja kwa moja ili waone umaana wa uwepo wa raslimali hii katika mazingira yao,” alisema Biteko.

Aliongeza kuwa, ni wajibu wa GGM kuwaeleza wananchi fursa zilizopo na namna mgodi unavyowashirikisha ili madini yanapokwisha   wananchi wabaki na kumbukumbu ya uwepo wa dhahabu hapa mkoani humo.

Pia, Waziri Biteko alitaka baada ya mkutano huo kuwe na maazimio yatakayo ratibiwa na kusimamiwa na Mkuu wa Mkoa  huku akisisitiza maazimio hayo kueleza  namna mgodi huo unavyokwenda mkieleza namna mnavyokwenda kuwahusisha wananchi.

Kwa upande mwingine, Waziri Biteko amekemea vikali vitendo vya udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu wanaopewa fursa ya kufanya biashara na migodi na kueleza kwamba, amekuwa akipokea malalmiko ya udanganyifu na wizi kwenye migodi unaofanywa na baadhi ya wasio wema na amewataka kubadilika na kutenda haki ili kuongeza imani ya kuendelea kuwatumia watoa huduma wa ndani.

Waziri Biteko alisema kuanzia sasa Kamishna Msaidizi anaye shugulikia masuala ya  Ushiriki wa Nchi na Wananchi katika Sekta ya Madini (Local Content) kutoka ofisi ya Kamishna wa Madini atakuwa anapita kukagua namna utekelezaji wa masuala ya Local content yanavyo tekelezwa na hii sio kwa mgodi wa GGM peke yake bali kwa migodi yote hapa nchini.

Pamoja na kuelezwa kuwa mpaka sasa mgodi wa GGM una asilimia 97 ya wafanyakazi ni wazawa, bado haitakuwa na maana kama maamuzi ya mambo mbalimbali yatakuwa yanasubiri asilimia 3 ya wafanyakazi wanaotoka nje.

Halikadhalika, Waziri Biteko aliwakumbusha watendaji wote wa Wizara ya Madini na Taasisi zake zote kuhusu agizo alilolitoa akiwa ziarani Mkoani Lindi wiki mbili zilizopita kuendelea kufuatilia yanayojiri kwenye ziara zake hususani viongozi kwani patafika mahali wananchi  na wadau watatakiwa kupatiwa  majibu ya papohapo ili kuondokana na kero bila kusubiri muda mrefu. Hivyo, alimtaka kila mtendaji kuwa tayari kupokea simu pindi atakapo muhitaji na kutolea majibu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alisema bado kwenye mgodi wa GGM kuna “figisu figisu” katika kuwapatia ajira wana Geita kwa visingizo mbalimbali na hususan ujuzi wa lugha ya Kiingereza  na kuwataka kubadilika katika hilo.

“Kuna figisu figisu ya utoaji wa ajira pale mgodini, moja ya sababu mnasema lugha, hicho Kiingereza sio ndio kinachofanya kazi, hiyo lugha sioni ulazima wake na sio wakati wote watakuwa wanaongea muda mwingi ni wakufanya kazi wakiwa wenyewe hata kisukuma watakuwa wanaimizana kufanya kazi,” alisema Mhandisi Gabrile.

Naye. Meneja Mkuu wa Mgodi wa GGM Richard Jordinson alisema kama mgodi wamedhamiria kuifanya jamii ya Geita kuwa sehemu ya mgodi na ndiyo sababu tayari wamewisha sainishana mikataba mbalimbali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Na kuongeza,  ni dhamira yao kuiona Geita yenye dhahabu inakuwa na  nuru ya dhahabu na wako tayari kushirikiana na jamii na serikali, kutii mamlaka za  serikali na kufuata marekebisho yote yaliyofanywa kwenye sheria ya madini na ndio maana  wameamua kukutana na wadau ili wajadili masuala yote.

Aidha, Uongozi wa GGM umemshukuru Waziri Biteko na wafanyakazi wote wa wizara kwa ushirikiano  wanao upata mara kwa mara kwani wanaifanya kazi yao kuwa rahisi, mara zote wamekuwa wakijadiliana na kukubaliana katika masuala mbalimbali.

Afisa Mtendaji Mkuu wa  Kampuni ya Anglo Gold Ashanti  Bara la Afrika, Sicelo Ntuli alisema mgodi GGM mwaka 2018 ulitenga bilioni 9.2 kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa mkoa wa Geita peke yake na wanatarajia kuanza kutekeleza miradi hiyo mwaka wa fedha wa  2019/20.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals