[Latest Updates]: STAMICO Yazinadi Fursa za Uwekezaji Sekta ya Madini Zilizopo Nchini Katika Maonesho ya Chama Cha Watafiti na Wawekezaji Sekta ya Madini Canada (PDAC) 2024

Tarehe : March 11, 2024, 1:30 p.m.
left

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse amezinadi fursa za uwekezaji katika sekta ya madini zilizopo nchini katika Maonesho ya Chama Cha Watafiti na Wawekezaji Sekta ya Madini Canada (PDAC) 2024 yaliyofanyika tarehe 3 hadi 6 Machi, 2024 jijini Toronto Canada. 

Dkt Mwasse amebainisha fursa hizo wakati akitoa mada kupitia MineAfrica Inc kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini kwa wadau wenye nia ya kuifahamu Sekta ya Madini Tanzania.

Alifafanua kuwa fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini nchini ni utafutaji na uchimbaji wa madini muhimu na mkakati wa uanzishaji wa viwanda vya kuongezaji thamani na biashara ya madini. Ilieleza  kuwa fursa hizo zinapatikana kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushirikiana na STAMICO. 

Dkt. Mwasse ametumia fursa ya maoneshio hayo kukaribisha wawekezaji kushirikiana na STAMICO kwa kufanya ubia katika baadhi ya leseni za madini mkakati ambazo Shirika inamiliki kama  lithium, iron ore, nickel, cobalt, graphtie, REE na copper. 

Amewahakikishia wawekezaji watakaoshirikiana na STAMICO kunufaika na uzoefu wa Shirika wa zaidi ya miaka 50 kwa rig za kisasa inazomiliki na shirika  ukaribu na wananchi na uelewa wa ufuatiliaji vibali nchini.

Pamoja na walisho hilo Dkt. Mwasse alitumia fursa hiyo kukutana  na Bw. Thomas Ulm Mkurugenzi wa Multipower Products ya Canada inayojihusisha na  kutengeza mitambo wa kuchoronga miamba. 

Mazungumzo hayo yalilenga kujadili hatua za usafirishaji wa mtambo wa uchorongaji ulioagizwa na STAMICO ambapo Bw. Thomas Ulm alieleza kuwa Mtambo huo umekamilika na umeshasafirishwa mwishoni mwa Februari 2024.

Maonesho haya yalishirikisha wataalamu mbalimbali kutoka Tanzania akiwemo Kamishna Msaidizi Undelezaji Migodi Bw. Terence Ngole pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya madini na Taasisi zake.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals