[Latest Updates]: Wizara ya Madini Yaendesha Kliniki ya Madini Songwe

Tarehe : July 3, 2024, 1:46 p.m.
left

●Yashirikisha Taasisi mbalimbali za Umma.

● Maeneo yatengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo

●Changamoto mbalimbali zaibuliwa.

SONGWE

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa leo Julai  3, 2024 amekutana na wachimbaji wadogo, wachenjuaji na wafanyabiashara wa madini Mkoa wa Songwe na kupokea changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza katika mkutano huo ambao umefanyika katika kijiji cha Saza Wilayani Songwe, Dkt. Kiruswa amesema kuwa Wizara ya Madini na taasisi zake imeanzisha kliniki ya madini kwa wachimbaji wa madini nchini kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji ndani ya sekta pamoja na sekta zinazofungamana na sekta ya madini ikiwemo sekta ya Nishati.

Dkt. Kiruswa amefafanua kuwa, Serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika Pato la Taifa hivyo ipo kila sababu ya kufahamu changamoto zinazowakabili na kutengeneza mkakati endelevu wa kuzitatua kwa kushirikiana  na sekta zinazofungamana na sekta ya madini.

Awali, akielezea hali ya uzalishaji wa madini ya dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo na wachenjuaji, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Songwe Chone Malembo,  amesema kuanzia Julai 2023 mpaka Julai 2024 kiasi cha kilogramu 1,059.35 zimezalishwa kutoka kwa wachimbaji wadogo.

Akielezea kuhusu mkakati uliopo, Malembo  ameeleza kuwa ofisi inaendelea kubainisha maeneo yaliyo wazi na kuangalia leseni za utafiti ambazo hazifanyiwa kazi ili kutoa mapendekezo maeneo yanayofaa kuwapatia wachimbaji wadogo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa  Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini Mkoani Songwe  (SOREMA), Emmanuel Kamaka amebainisha changamoto zinazowakabili wachimbaji ikiwa pamoja na ukosefu wa nishati ya umeme ya uhakika, utitiri wa kodi katika mnyororo mzima wa madini , utoaji wa leseni katika maeneo yanayofanyiwa kazi kwa pamoja zinasababisha uchimbaji kuwa mgumu.

Kuanza kwa Kliniki ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio yaliyotolewa wakati wa mkutano mkuu wa mwaka 2024 wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) ambapo kliniki hiyo imejumuhisha wataalam kutoka taasisi mbalimbali za Umma ikiwemo TANESCO, GST, STAMICO, NEMC, TRA, Mkemia  Mkuu wa Serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Songwe.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals