Tarehe : Nov. 12, 2018, 8:51 a.m.
Na Samwel Mtuwa, GST
Watalaam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania-GST) tarehe 10 Oktoba 2018 walikutana na watalaam kutoka Taasisi ya Jiolojia ya China (Geological Survey of China-CGS) kwa ajili ya uwasilishaji na upokeaji wa taarifa ya mradi wa Utafiti wa Jiokemia katika skeli kubwa na skeli ndogo yaani (Geochemical Mapping for High and Low Density) uliofanyika kwa ushirikiano baina ya Serikali ya China na Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST, Yokbeth Myumbilwa alisema kuwa, Utafiti huo umekusanya taarifa mbalimbali katika upande wa low density na high density ambapo kwa upande wa low density utafiti ulifanyika katika Mikoa ya Mbeya na Songwe na high density ulifanyika kwa nchi nzima .
Akizungumzia juu ya faida zitokanazo na mradi huu wa ushirikiano , Myumbilwa alieleza baadhi ya malengo ya mradi kuwa ni kupata taarifa za utafiti wa jiokemia kwa ajili ya kuandaa kanzidata ambayo itaainisha uwepo wa taarifa za jiokemia za nchini zitakazo ainisha uwepo wa aina mbalimbali za madini, upangaji miji ,pamoja na taarifa hizo kuweza kutumika katika shughuli mbali mbali ndani ya sekta ya killimo na mazingira.
Alisema kuwa, faida nyingine ni upatikanaji wa taarifa ambazo zitasaidia pia kuanisha aina mbalimbali za udongo kwa njia ya Ramani yaani (Geochemical Atlas Map of Tanzania).
Mnamo mwaka 2009 serikali ya China na Tanzania kwa kutumia taasisi zake za Geological Survey zilisaini hati ya makubaliano (MoU) kwa lengo la kuanzisha mradi huu wa miaka mitano ambapo kazi rasmi ya mradi ilianza mwaka 2013mpaka 2018.
Akizungumza wakati wa kufunga hafla hiyo, Myumbilwa alishukuru kwa mafanikio makubwa ya mradi huo , pamoja ushirikiano mzuri uliokuwepo wakati wa utekelezaji wa mradi toka ulipoanza mwaka 2013.
Katika hafla hiyo ya upokeaji wa taarifa GST iliwakilishwa na watalaam 11 na upande wa China CGS uliwakilishwa na watalaam Sita Sun Xiaoming ambaye ni mkurugenzi wa CGS, Sun Kai , Wang Huichu , TengXuegian , Li Janjian , Liu Xiaoyangi na Gong Kenghui.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.