[Latest Updates]: Tumejipanga Kuvuka Lengo la Ukusanyaji wa Maduhuli Kwa Mwaka 2020-2021- Tume ya Madini

Tarehe : Dec. 14, 2020, 12:22 p.m.
left

Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Madini, William Mtinya amesema kuwa Tume imejipanga katika kuhakikisha inavuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2020-2021 la shilingi  bilioni 526.

Mtinya ameyasema hayo leo Desemba 14, 2020 jijini Dodoma kupitia mahojiano maalum kwenye kikao kazi cha Tume ya Madini ambacho kinakutanisha Wakurugenzi na Mameneja kutoka Makao Makuu ya Tume ya Madini pamoja na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa na  Maafisa Migodi Wakaguzi.

Amesema kuwa ili kuhakikisha lengo la ukusanyaji wa maduhuli linafikiwa, Tume ya Madini imeweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na udhibiti wa utoroshaji wa madini kupitia masoko na vituo vya ununuzi wa madini vilivyowekwa, kuongeza vitendea kazi kwenye masoko ya madini na kuweka mazingira bora kwenye usimamizi wa shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini.

Katika hatua nyingine amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na uwekezaji kwenye Sekta ya Madini, kampuni za uchimbaji wa madini zinatakiwa kuwa na mipango ya ushirikishwaji wa watanzania kwenye Sekta ya Madini pamoja na kuitekeleza.

“Katika utekelezaji wa mipango hii wawekezaji wanatakiwa kuhakikisha wanatoa ajira kwa watanzania na kununua bidhaa kutoka kwa watanzania ili kila mwananchi  anufaike kwa namna moja au nyingine” amesema Mtinya.

Lengo la kikao ni pamoja na kujadili changamoto mbalimbali kwenye utekelezaji wa majukumu pamoja na kuzipatia ufumbuzi. Aidha watendaji watajifunza namna ya kuandaa bajeti inayoendana na Mpango Kazi wa Tume ya Madini na namna ya  kuitekeleza

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals