[Latest Updates]: Naibu Waziri Mkuu Aipongeza Tume ya Madini kwa Ukusanyaji wa Maduhuli

Tarehe : Oct. 5, 2024, 1:53 p.m.
left

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amepongeza Tume ya Madini kwa kuendelea kuvuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli na kusisitiza kuendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha wanavuka lengo walilopewa na Serikali la kukusanya kiasi cha shilingi Trilioni Moja katika mwaka wa fedha 2024/2025.

Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Oktoba 05, 2024 alipotembelea banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake akiwa ameambatana na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde katika Maonesho  ya Saba ya Kitaifa ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Geita yaliyoanza Oktoba 2, kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

"Mnafanya kazi nzuri sana Tume ya Madini, lengo mlilopewa ni kukusanya Shilingi  Trilioni Moja katika mwaka wa fedha 2024/2025, naamini mtalivuka," amesema Dkt. Biteko.

Taasisi nyingine chini ya Wizara ya Madini zinazoshiriki katika maonesho ni pamoja na  Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia ( TEITI),  Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania ( GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals