[Latest Updates]: Nyongo aifungia kampuni ya uchakataji madini bati isiyo na leseni

Tarehe : April 28, 2018, 2:41 p.m.
left

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amemwagiza mmiliki wa Kampuni inayochakata Madini Bati ya African Top Minerals iliyopo Kyerwa mkoani Kagera, Hassan Ibar, kutoendelea na kazi hiyo hadi pale atakapofuata taratibu za kuomba na kupatiwa leseni halali ya Serikali.

Ujumbe wa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo wakikagua shimo linalochimbwa Madini ya Bati katika Mgodi wa Hamad Mine Scale, uliopo eneo la Omukasheni, Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Februari 28 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi.[/caption]

Alitoa agizo hilo jana Februari 28, alipotembelea na kukagua Kampuni hiyo akiwa katika ziara yake ya kazi mkoani Kagera.

Naibu Waziri alimwambia mmiliki huyo kuwa, Serikali inapenda wawekezaji wawepo ili pamoja na mambo mengine wasaidie upatikanaji wa ajira kwa wananchi lakini akaonya kwamba kamwe haitaridhia mtu yeyote kufanya uwekezaji pasipo kuwa na leseni halali itakayowezesha kutambuliwa na Serikali na kulipa kodi zote stahiki.

“Naomba utambue kuwa unafanya shughuli hii kinyume cha sheria. Hivyo naagiza, kuanzia sasa usiendelee na kazi hadi pale utakapokuwa na leseni.”

Aidha, Naibu Waziri pia alitembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kyerwa kuliko na shughuli za uchimbaji madini ya Bati pamoja na Viwanda kadhaa vya uchakataji Madini hayo, vikiwemo vya TanzaPlus Minerals na Hamad Mine Scale.

Akizungumza na wana-kikundi wa Umoja wa Wachimbaji Kyerwa, Naibu Waziri aliwasihi wawe wavumilivu wakati Serikali ikishughulikia suala la kujisajili na Mikataba ya Kimataifa itakayowezesha kutambulika kwa Madini ya Bati yanayochimbwa nchini ili yaweze kuuzwa popote Duniani.

“Natambua mnapitia kipindi kigumu kutokana na zuio tuliloweka la kutouza Madini ghafi nje ya nchi. Serikali inashughulikia suala hilo kwa uharaka ili kama nchi, nasi tuweze kuingia katika Mikataba hiyo ya Kimataifa ambayo itatuwezesha kuleta wawekezaji mbalimbali hapa, waje wanunue madini yetu hapa kwa ushindani, na tuuze kwa bei nzuri zaidi tofauti na ilivyo sasa.”

Mmoja wa wamiliki wa Mtambo wa kuchenjua Madini ya Bati wa TanzaPlus Minerals, Salim Mhando (kushoto), akimwonesha Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa pili kutoka kushoto), moja ya mashine zinazotumika kuchakata Madini hayo. Naibu Waziri alitembelea na kukagua Mtambo huo uliopo Nyaluzumbulwa wilayani Kyerwa, Mkoa wa Kagera, Februari 28 mwaka huu.[/caption]

Hata hivyo, Naibu Waziri aliwataka wachimbaji hao kuachana na suala la utoroshaji wa madini na kuyauza kwa njia za magendo huku akionya kwamba, yeyote atakayekamatwa, atawajibika kisheria.

Awali, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali Shaban Lissu, Naibu Waziri alimsisitiza kuhakikisha Ofisi yake inaimarisha ulinzi katika njia zote za panya, ili kudhibiti utoroshwaji wa madini.

Kwa upande wao, wachimbaji wadogo wa Kyerwa, wakiwasilisha maombi yao kwa Serikali, walimwomba Naibu Waziri kupatiwa leseni katika maeneo mbalimbali.

Akijibu maombi hayo, Naibu Waziri aliwaahidi kuwa Leseni zitaanza kutolewa na kuhuishwa mara tu Tume ya Madini itakapoanza kufanya kazi, ambapo alisema anaamini itakuwa ni hivi karibuni.

Imeandaliwa na:

Veronica Simba, Kagera

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals