Tarehe : March 4, 2025, 2:26 p.m.
#Kiwango cha makusanyo ya maduhuli ya Serikali kimepanda kutoka shilingi bilioni 624.61 zilizokusanywa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia shilingi bilioni 753.82 mwaka wa fedha 2023/2024
#Mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 7.2 mwaka 2021 hadi asilimia 9 mwaka 2023 kutokana na kuimarika kwa usimamizi wa shughuli mbalimbali za madini.
#Ukuaji wa sekta ya madini umeongezeka kutoka asilimia 9.4 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 11.3 mwaka 2023.
#Ukuaji wa sekta ya madini na mchango wake katika Pato la Taifa unatarajiwa kufikia asilimia 10 na zaidi ifikapo mwaka 2025.
#Kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 mauzo ya madini katika masoko na vituo vya ununuzi wa madini yameendelea kuongezeka kutoka shilingi bilioni 2.361.80 hadi shilingi bilioni 2,597.18 kwa mwaka 2023/2024.
#Tume ya madini imeendelea kusimamia kikamilifu upatikanaji wa ajira kwa Watanzania kwenye kampuni mbalimbali za uchimbaji wa madini.
#Ajira 19,874 zimezalishwa na makampuni ya uchimbaji wa madini ambapo kati ya hizo, 19,371 ni Watanzania.
#Tume ya madini imeendelea kutenga maeneo mahsusi kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
#Tume imefanikiwa kutenga maeneo 58 kwa ajili ya wachimbaji wadogo katika mikoa mbalimbali.
#Tume imeweka mazingira rafiki kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini kupata leseni za uchimbaji pamoja na kuwaunganisha na taasisi za kifedha ili wapate mikopo kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli za uchimbaji.
#Tume imefanikiwa kutoa jumla ya leseni 41,424 kati ya 37,318 zilizopangwa kutolewa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo ni sawa na asilimia 111. Leseni hizo zilijumuisha leseni za uchimbaji mkubwa, uchimbaji wa kati na uchimbaji mdogo.
#Sekta ya madini ni miongoni mwa sekta muhimu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.