[Latest Updates]: Wizara ya Madini Kushiriki Mkutano wa Madini Mkakati Ufaransa

Tarehe : Sept. 27, 2023, 8:09 a.m.
left

Paris

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa umewasili nchini Ufaransa  kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Usalama wa Madini  Mkakati  utakaofanyika kesho Septemba 28, 2023.

Mkutano huo unatazamiwa kujadili masuala muhimu kuhusu madini mkakati, kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili namna ya kushiriki katika kuchochea usimamizi na usambazaji endelevu wa madini hayo.

 Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Kimataifa inayoshughulika  na masuala ya Nishati Safi (International Energy Agency-IEA).

Aidha, mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri, Wafanyabiashara, Wawekezaji, taasisi za kimataifa na taasisi za kiraia.

Mbali na Naibu Waziri, wengine wanaoshiriki kutoka Wizara ya Madini ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo, Kamishna Msaidizi wa Madini  sehemu ya Uendelezaji Migodi kutoka Wizara ya Madini, Terence Ngole, Kaimu Mkurugenzi wa Kanzidata kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania ( GST) Hafsa Seif .
 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals