[Latest Updates]: Waziri Mavunde Apokea Changamoto za Wachimbaji Wadogo Itumbi

Tarehe : Oct. 29, 2023, 5:56 p.m.
left

# Ni ukosefu wa Mitaji , Nishati ya Umeme na Vifaa duni vya uchimbaji

# Ubovu wa miundombinu ya Barabara katika migodi

Wizara ya Madini - Chunya.

Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde apokea changamoto mbalimbali za wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wilayani Chunya mkoani Mbeya katika machimbo ya Itumbi akiwa katika ziara maalum ya kikazi.

Waziri Mavunde akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Ndugu Mayeka Simon Mayeka alipokelewa na wachimbaji zaidi ya 200 ambao katika mkutano walitaja changamoto zao mbalimbali kama vile ukosefu wa mitaji , vifaa duni vya uchimbaji , ukosefu wa Nishati ya Umeme na kukosekana kwa  Miundombinu salama.

Mapema baada ya kupokea changamoto hizo Mhe.Mavunde aliwatoa hofu wachimbaji kwa kuwaambia kuhusu mikakati mbalimbali iliyowekwa na Serikali katika kuwainua wachimbaji wadogo nchi nzima kwa kuwapatia mashine za uchorongaji,kuwaunganisha na Taasisi za fedha ili kupata mikopo yenye riba nafuu na mpango wa kufanya utafiti wa kina ili kupata taarifa sahihi za miamba na madini.

Mhe.Mavunde amewataka wachimbaji wa Itumbi kujiunga na kujisajili rasmi katika vikundi ili watambulike  na kuwekwa katika mikakati ya serikali itayowawezesha kujengewa 
uwezo na kutatua changamoto zao.

Mhe .Mavunde amemuagiza Afisa Madini Mkazi Chunya ndugu Sabahi Nyansiri kusimamia na kuratibu zoezi hilo la kuunda vikundi  na kuvisajili katika mifumo rasmi ili vitambulike na mamlaka husika.

Soko la Madini Wilayani Chunya lilianzishwa Mei 2, 2019. Kabla ya soko kuanza dhahabu iliyokuwa  ikionekana katika takwimu za Serikali ni 
kilogramu 20 na baada ya soko kuanza wastani wa dhahabu inayopatikana kwa mwezi ni zaidi ya kilogramu 250.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals