Tarehe : March 10, 2022, 12:42 p.m.
Chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, mchango wa Sekta ya Madini katika pato la taifa umekuwa ukiongezeka kutoka robo moja ya mwaka hadi nyingine
Katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2021 wastani wa mchango wa sekta hii umekuwa hadi kufikia asilimia 7.3 ya Pato la Taifa ikilinganishwa na wastani wa asilimia 6.5 Katika kipindi kama hicho mwaka 2020.
Sekta ya Madini imeweka historia kwa kushuhudia mauzo ya moja kwa moja yenye thamani ya shilingi trillioni 8.3 kutokana na mauzo ya madini ya aina mbalimbali.
Wizara imekusanya shilingi bilioni 597.53 kama maduhuli ya Serikali.
Ushiriki wa Watanzania kwenye shughuli za madini umekuwa kutoka asilimia 48 hadi asilimia 63 na hivyo kuongeza thamani ya huduma migodini kufikia thamani ya Dola za Marekani Milioni 579.3 sawa na Shilingi Trilioni 1.33.
Wizara ya Madini imeanza ushirikiano na Wizara ya TAMISEMI ili kuweza kuwafikia wananchi wanaotumia madini hayo waweze kuchangia fedha zitokanazo na shughuli za uchimbaji madini kwa mujibu wa Sheria ya Madini.
# Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhesimiwa Samia Suluhu Hasan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kusimamia na kuhakikisha wachimbaji wadogo wanashiriki kikamilifu na kwa ufanisi kwenye uzalishaji madini hapa nchini.
Katika awamu hii tumeshuhudia utoaji wa leseni mbalimbali kwenye shughuli za madini ukiongezeka.
Jumla ya leseni 8,172 zimetolewa, kati ya leseni hizo, leseni 5,937 ni za uchimbaji mdogo wa madini, leseni 282 ni za utafutaji wa madini, leseni 5 ni za uchimbaji wa kati wa madini, leseni 2 ni za uchimbaji mkubwa wa madini, leseni 49 ni za uchenjuaji wa madini, leseni 2 ni za usafishaji wa madini;
Aidha leseni 1,531 ni za biashara ndogo ya madini na leseni 364 kubwa za biashara ya madini zilitolewa kwa wawekezaji na wananchi, ikilinganishwa na jumla ya leseni 6,334 zilizotolewa katika kipindi cha kuanzia Machi 2020 mpaka hadi Februari 2021.
#Katika mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani, kwa mara ya kwanza katika historia ya Sekta ya Madini, Serikali ilifanikiwa kusaini mikataba mipya minne ya uchimbaji na uanzishwaji wa migodi mikubwa na ya kati ya madini kwa wakati mmoja.
Kupitia Maonesho Makubwa ya Biashara ya Dubai Expo2020 Serikali kupitia STAMICO hivi karibuni imesaini mkataba wa uchorongaji kati yake na Buhemba Gold Company wenye thamani ya shilingi bilioni 11.5.
Serikali ya Awamu ya Sita ilitoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 11.28 ili kuiwezesha Tume ya Madini kufanya ununuzi wa magari pamoja na vifaa vya masoko kwa lengo la kuboresha utekelezaji wa majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na rasilimali madini.
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), imefanikiwa kusogeza karibu huduma za maabara kwa wachimbaji wadogo wa madini kwa lengo la kuwasaidia wachimbe kisayansi na hivyo kuongeza tija na mapato ya serikali.
# Majukumu mengine yaliyotekelezwa na wizara katika uongozi wa Serikali ya Awamu ni pamoja na kufanyika kwa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini ulishirikisha washiriki wapatao 1,200 kutoka ndani na nje ya nchi na wengine kushiriki kwa njia ya mtandao.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.