Tarehe : July 11, 2024, 3:26 p.m.
Wananchi wanaotembelea Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam wavutiwa na Mkaa Mbadala wa Rafiki Briquettes unaotengenezwa kwa kutumia madini ya makaa ya mawe na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)
Kutokana na shauku hiyo wameiomba STAMICO kuongeza wigo wa usambazaji mkaa mbadala huo ndani na nje ya mipaka ya nchi ili kuwafikia watumiaji wengi.
Akitoa maoni yake mara baada ya kupata elimu ya umuhimu wa kutumia mkaa mbadala wa mkaa utokanao na miti Bw. Isaac Katogo amesema mkaa huu ni mzuri na ni sehemu ya kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji.
Naye, Bw. Emmanuel Kayoka amesema teknolojia ya mkaa Mbadala imekuja wakati muafaka ambapo dunia na Taifa vipo katika jitihada ya kuzuia uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti.
"Niwapongeze STAMICO kwa kuja na Mkaa huu ambao umelenga kuongeza chachu ya kuhamasisha utunzaji wa uoto wa asili (misitu) na kuhakikisha mazingira yanabaki salama" alisema Bw. Kayoka
STAMICO imeendelea kutumia fursa mbalimbali kuhamasisha matumizi ya mkaa mbadala sambamba na kuongeza uzalishaji kwa kusimika mitambo mikubwa miwili ya kuzalisha mkaa huo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.