[Latest Updates]: Wananchi Wapongeza Mgodi wa Mundarara

Tarehe : March 24, 2024, 9:11 a.m.
left

●Wafurahishwa na utekelezaji wa CSR.

Arusha

WANANCHI wanaozunguka mgodi wa Mundarara unaochimba madini ya Rubi uliopo katika Kijiji cha Mundarara, tarafa ya Engarenaibor , Wilaya ya Longido mkoani Arusha wameupongeza Mgodi huo kwa kuwaletea maendeleo ya  kiuchumi na kijamii pamoja na kuwashirikisha katika shughuli za uchimbaji madini.

Hayo yamebainishwa  Machi 23, 2024 na wananchi hao kwa waandishi wa habari wanaofanya ziara ya kutembelea Mgodi huo kwa lengo la kujionea shughuli za uchimbaji madini.

Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wa Mgodi huo Leita Mollel amesema kuwa Mgodi wa Mundarara umekuwa mkombozi katika maisha yao ambapo kupitia Mgodi huo wananufaika na huduma mbalimbali.

Akitolea mfano baadhi ya huduma hizo ni pamoja na kupata ajira, kupata mchanga wa madini,ujenzi wa madarasa , uboreshaji wa makazi kupitia biashara ya madini wanayofanya mgodini hapo.

Kwa upande wake , Meneja wa Mgodi Frank Luholela amesema kuwa mgodi unaendelea kutekeleza kanuni ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) hususani katika masuala yanayohusu maendeleo ya jamii.

Luholela ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu  ya uchimbaji, mgodi umeendelea kutoa ushirikiano kwa wananchi wanaouzunguka kwa kuwapatia mifuko ya mawe ya madini yanayochimbwa katika  mgodi ambapo huchambua na kupata madini ambayo wanauza na kupata kipato.

Akielezea kuhusu maendeleo ya mgodi huo , Luholela ameeleza kuwa mgodi umefikia mita 320 kwenda chini ambapo kwa upande wa magharibi umeenda mita 500 na mashariki mita 100.

Mgodi wa rubi  Mundarara unamilikiwa na Shirika la Madini la Taifa  ambayo ipo  ubia na Kampuni inayojishulisha na uchimbaji madini ya vito ya  RGI.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals