[Latest Updates]: Kikao cha 21 cha Makatibu Wakuu wa Kituo cha AMGC chafanyika Tanzania

Tarehe : June 7, 2018, 11:30 a.m.
left

Makatibu Wakuu kutoka nchi Wanachama wa Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC) wameshiriki katika kikao cha 21 cha Kituo hicho kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akichangia mada katika kikao cha 21 cha Makatibu Wakuu kilichofanyika katika Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC) Kuduchi, jijini Dar es Salaam.[/caption]

Akifungua rasmi kikao hicho kilichofanyika tarehe 6-7 Juni, 2018, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Tanzania, Prof. Simon Msanjila ambaye anashiriki kwa mara ya kwanza, alisema kuwa, kituo hicho hakina budi kuweka jitihada katika kuhamasisha nchi  nyingine za Afrika ambazo bado hazijajiunga ili ziweze  kujiunga  na kituo hicho.

Pia, alieleza kuhusu umuhimu wa kituo kuendelea kuweka msisito kwa nchi wanachama kulipa ada za uanachama kwa wakati na kuhakikisha kuwa kinatekeleza majukumu yake kwa ubora uliokusudiwa.

Akichangi mada, Prof. Msajila alizungumzia kuhusu suala la upatikanaji wa eneo la ujenzi wa vinu vya kuchenjua na kuongeza thamani madini na kushauri kuhusu kuzingatia suala ya uhifadhi wa mazingira.

Pia, Profesa Msajila alikitaarifu kikao hicho kuhusu ushiriki wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka na Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amon Maganga pamoja na Wataalam mbalimbali kutoka taasisi hizo  katika Mkutano wa 38 wa Wakuu wa nchi wanachama utakaofanyika tarehe 8 Juni, 2018.

“ Nimeeleza kuhusu ushiriki wa Watendaji hao kwa lengo la kujadili suala la kufanya biashara na kituo cha AMGC kwa kuwa vipo vifaa ambavyo kituo chetu kinaweza kuvizalisha kwa matumizi ya taasisi za REA na TANESCO,” alisema Prof. Msanjila.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kikao hicho Dkt. Kojo Busia alisema kuwa, asilimia 75 ya madini ya Coltan hupita katika Bandari ya Dar es Salaam Tanzania kuelekea nchi jirani ukilinganisha na asilimia 25 ambayo hupita Mombasa nchini Kenya na kueleza umuhimu kituo hicho kuboreshwa ili kutoa huduma bora zaidi.

Mwenyekiti wa Bodi wa Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC), Assa Mwakilembe akichangia mada katika kikao hicho. Kulia kulia kwake Mjumbe kutoka nchi ya Uganda.[/caption]

Pia, Dkt. Busia alisisitiza suala la kituo cha AMGC kuona namna bora ya kuungana na Taasisi ya African Minerals Development (AMDC) ili kuwa chombo kimoja ambalo litapelekea kuongeza ufanisi wa kituo hicho.

Nchi wanachama wa kituo cha AMGC ni Tanzania, Angola, Msumbiji, Sudani Kaskazini, Ethiopia, Uganda, Kenya, Comoro na Burundi.

Imeandaliwa na:

Rhoda James, Dar es Salaam

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals