[Latest Updates]: Dkt. Kiruswa Atatua Mgogoro wa Wachimbaji Longido

Tarehe : Dec. 7, 2024, 7:26 p.m.
left

Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan haitaki migogoro katika sekta ya Madini

Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.

Longido,Arusha

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa ametatua mgogoro wa wachimbaji wadogo wa Madini ya Ruby Wilaya ya Longido Mkoani Arusha uliodumu zaidi ya miaka mitano kati ya Kampuni ya Paradiso Mineral (T) Limited na Mzee Malulu Ole Moringo kwa Kampuni hiyo kukubali kumlipa fidia Mzee Malulu Ole Moringo ya jumla ya shillingi milioni miamoja na hamsini ili kupisha shughuli za uchimbaji madini.
 
Makubaliano hayo yameafikiwa leo Desemba 6, 2025 wakati Mhe. Dkt. Kiruswa alipofanya ziara ya kutatua mgogoro huo katika Kata ya Mundarara Wilaya ya Longido Mkoani Arusha. 
 
Mhe. Dkt. Kiruswa ameielekeza kampuni ya Paradiso kutekeleza makubaliano walioafikiana na Mzee Malulu Ole Moringo ya kulipa fidia hiyo kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza wanatakiwa kulipa milioni 100 ifikapo Januari 30, 2025 na milioni 50 ifikapo Machi 30, 2025.
 
Aidha, Dkt. Kiruswa amesisitiza makubaliano hayo kutekelezwa kwa wakati na endapo kampuni ya Paradiso itakiuka makubaliano hayo Serikali itachukua hatua za kisheria ikiwemo kusimamisha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.
 
Sambamba na hayo, Dkt. Kiruswa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na  Dkt. Samia Suluhu Hassan haitaki migogoro katika sekta ya Madini ili sekta hiyo kuwa na  maendeleo.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Kiruswa amewataka wachimbaji wa madini kuendelea kulipa kodi za Serikali ambapo fedha hizo zitakwenda kuboresha huduma za kijamii kama vile kujenga shule na usambazaji wa umeme maeneo mbalimbali hapa nchini.

Awali, Ofisi ya Madini Arusha ilifanya utafiti na kugundua Malulu Ole Moringo ana haki katika eneo hilo ambalo familia ya Jango Master inafanya shughuli za uchimbaji Madini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha (CCM) Papaanakuta Moleli amempongeza Dkt. Kiruswa kwa kazi nzuri anazozifanya za kutatua migogoro mbalimbali ya wachimbaji wa Madini  hapa nchini.

Nayo, Familia  ya Jango Master ikiwakilishwa na Victor Jango imekubali kulipa fidia hiyo kwa wakati, huku Malulu Ole Moringo naye akiridhia kupokea fidia hiyo kama Serikali ilivyoelekeza.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals