[Latest Updates]: Tanzania Kushiriki Mkutano wa Mwaka wa PDAC 2025 Nchini Canada

Tarehe : March 2, 2025, 2:11 p.m.
left

Tanzania

Tanzania inatarajia kushirikia mkutano Mkuu wa mwaka 2025 wa jumuiya ya Watafiti na Wawekezaji wa Sekta ya Madini nchini Kanada (PDAC) unaotarajiwa kufanyika jijini Toronto kuanzia Machi 2 hadi 5 , 2025.

Katika Mkutano huu, Tanzania itawakilishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) , ambalo litakuwa miongoni mwa washiriki kupitia banda la MineAfrica Inc .

STAMICO itakuwa katika banda namba 923 lililo katika jengo la kusini katika kituo cha Mikutano cha Metro Toronto.

Ushiriki wa Tanzania kupitia STAMICO katika mkutano huu ni fursa muhimu ya kutangaza na kuvutia uwekezaji katika mnyororo mzima wa thamani madini.

Pamoja na mambo mengine, katika mikutano iliyopita , STAMICO imekuwa ikinadi na kutangaza fursa za uwekezaji katika madini ya metali hususan dhahabu na madini muhimu kama vile madini ya Lithium,Kinywe, Cobalt, Tina, chuma na madini ya Rare Earth Element (REE) kwa lengo la kuwakaribisha wawekezaji.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals