[Latest Updates]: Waziri Mavunde Awataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Kusimamia Sheria

Tarehe : Nov. 18, 2024, 12:39 p.m.
left

Awapongeza ukusanyaji wa maduhuli_

Asisitiza utatuzi wa migogoro kwa haraka
 
WAZIRI wa Madini, Mheshimiwa, Anthony Mavunde amewataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kuendelea kusimamia sheria kwenye utendaji kazi ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza kati ya wachimbaji wa madini na ajali kwenye shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini.
 
Waziri Mavunde ametoa rai hiyo kwenye kikao kazi cha menejimenti ya Tume ya Madini kilichofanyika mapema leo Novemba 18, 2024 chenye lengo la kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha Sekta ya Madini kuanzia kwenye ukusanyaji wa maduhuli, usimamizi wa sheria, biashara ya madini na mchango wake kuendelea kukua kwenye Pato la Taifa.
 
Amesema kuwa kuendelea kusimamia sheria katika utendaji kazi kumewasaidia Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa wengi kuwepo hapa leo hii.

 
Katika hatua nyingine amepongeza kasi ya ukusanyaji wa maduhuli inayofanywa na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa na kuwataka kuendelea kuwa wabunifu hasa kwenye udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato.
 
Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amewaagiza wakaguzi migodi  kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye migodi hususan kipindi hiki cha mvua ili kuepusha majanga migodini.
 
“Kuanzia kipindi hiki mpaka Aprili mwakani ni kipindi cha mvua, mfanye ukaguzi mara kwa mara, migodi isiyoridhisha ifungiwe hadi itakapoboreshwa, hatutavumilia vifo vya uzembe migodini,”amesema Mhandisi Samamba.
 
Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo amewataka   Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kutimiza  majukumu yao ​sio tu kufikia lengo la  Shilingi Trilioni moja, malengo yapo mengi na makubwa na kwamba sekta ya madini inatakiwa kuchangia kwenye pato la Taifa kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025
 
“Tufanye udhibiti wa kutosha, tukasimamie sheria, kanuni na taratibu tutafikia mchango wa asilimia  10 na kuzidi,”amesisitiza Mbibo.
 
Katika hatua nyingine, Mbibo ameelekeza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kuangalia namna bora ya kudhibiti mianya ya utoroshaji wa madini  hasa kwenye maeneo ya mipakani na viwanja vya ndege.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals