[Latest Updates]: Wizara ya Madini Kuibuka na Miradi Mikubwa ya Kimkakati

Tarehe : Aug. 13, 2024, 1:09 p.m.
left

Dodoma

Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Kampuni mbalimbali za uchimbaji na uchakataji madini inatarajia kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati itakayohusisha mnyororo mzima katika Sekta ya Madini.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 13, 2024 jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Ramadhan Lwamo wakati akiwasilisha taarifa kuhusu hali ya ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaopaswa kutoa maeneo yao ili kuruhusu uendelezaji wa leseni za uchimbaji wa madini nchini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Mhandisi Lwamo amesema kuwa Tume ya Madini ilitoa Leseni za Uchimbaji wa Madini wa Kati na Mkubwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo yamekuwa yakihitaji taratibu za kuhamisha wananchi ili kupisha utekelezaji wa miradi husika.

Aidha, Mhandisi Lwamo ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa uchimbaji madini ya nikeli wa Kabanga, Mradi wa uchimbaji mkubwa wa SMCL mkoani Mwanza, Mradi wa uchimbaji madini ya Kinywe wa Faru Graphite  mkoani Morogoro, Mradi wa uchimbaji madini ya mchanga mzito wa Baharini (Heavy mineral sands).

Vilevile, Mhandisi Lwamo ameitaja miradi mingine ni pamoja na Mradi wa uchimbaji madini ya Kinywe wa Bunyu, Nachu na Chilalo mkoani Lindi na Epanko mkoani Morogoro.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa Wizara ya Madini inaahidi kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha Kampuni zinakamilisha taratibu za ulipaji wa fidia kwa wananchi pamoja na kuendeleza miradi husika na kusimamia utekelezaji wake.

Waziri Mavunde ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa ushauri wake makini ambao imekuwa ikiutoa katika nyakati tofauti na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo na ushauri wote wa Kamati hiyo katika kuhakikisha sekta ya madini inaendelea kukua kwa kasi na hatimaye kuchangia ipasavyo katika ukuaji wa uchumi wa Taita.

#Vision2030 #MadiniNiMaishaNaUtajiri #InvestInTanzaniaMiningSector

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals