[Latest Updates]: Tanzania Yanadi Fursa za Uwekezaji, Ushirikiano Sekta ya Madini na Shirika la Nasr Kutoka Iran

Tarehe : Feb. 21, 2024, 8:17 p.m.
left

Waanza mazungumzo na STAMICO kununua Madini ya Chuma, Jasi, Lami na Makaa ya Mawe

Wizara ya Madini imenadi fursa za uwekezaji na ushirikiano wa kibiashara kwa Shirika la Nasr Corporation Group kutoka nchini Iran ambalo limeonyesha nia ya kununua baadhi ya Madini kutoka hapa nchini.

Hayo yamebainishwa katika kikao cha pamoja  baina ya Wizara ya Madini ikiambatana taasisi zake ikiwemo Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Tume ya Madini na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Shirika hilo la Nasr Corporation Group kilichofanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na Wataalam kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). 

Ujumbe wa Wizara ya Madini umeongozwa na Kamishna Msaidizi wa Madini Maruvuko Msechu ambapo amesema kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini imekuwa ikifanya programu kadhaa ambazo ni pamoja na kuandaa na kutekeleza sera na taratibu za maendeleo ya madini zilizoboreshwa; kuweka sheria na kanuni madhubuti za usimamizi wa sekta pamoja na mfumo madhubuti wa kitaasisi; kutunga utaratibu wa kifedha unaoruhusu kuvutia uwekezaji wa umma na binafsi katika sekta na kuvutia uwekezaji wa kimataifa.

Ujumbe huo pia umefanya wasilisho la fursa za ushirikiano katika Sekta ya Madini ambako Mkurugenzi wa Huduma za Kijiolojia Kutoka GST, Dkt. Ronald Massawe ameeleza  fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini hapa nchini na kuongeza kuwa hivi sasa kazi kubwa inayofanyika ni majaribio ya utafiti wa kina wa Jiosayansi ili kubaini maeneo yote yenye rasilimali madini hapa nchini.

Kwa upande wake, Mtaalam kutoka STAMICO Dennis Semeo ameeleza maeneo ambayo wanaweza kushirikiana na Shirika la Nasr katika uwekezaji ikiwa ni pamoja na kufanya biashara ya kuuza na kununua madini kama vile makaa ya mawe, madini ya viwandani, madini ya ujenzi pamoja na Madini Mkakati na Muhimu ambayo uhitaji wake ni mkubwa sana hivi sasa duniani. 

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jihad Nasr ambayo ni sehemu ya Shirika la Nasr, Reza Azimi amesema kuwa Shirika hilo linalojihusisha na shughuli za Ujenzi, Viwanda na Uchimbaji na Kilimo limevutiwa na fursa za ushirikiano na kibiashara zilizopo Tanzania na kuongeza kuwa Shirika lake limevutiwa zaidi biashara ya kununua madini chuma, makaa ya mawe, jasi na lami (bituminous) kutoka Tanzania. 

Mazungumzo kati ya STAMICO na Nasr yanaendelea wakati wakisubiri Mkataba wa Makubaliano- (MoU ) kuhusu jinsi biashara ya madini hayo itakavyofanyika baina ya Mashirika hayo mawili.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals