[Latest Updates]: Serikali Yaimarisha Uwezeshaji wa Wachimbaji Wadogo Nchini - Dkt. Kiruswa

Tarehe : Feb. 14, 2025, 5:45 p.m.
left

 Dodoma

Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imesaini Hati za Makubaliano (MoU) na Kampuni za GF Truck, Apollo Heavy Equipments, na META kwa lengo kurahisisha upatikanaji wa mitambo ya kisasa kwa wachimbaji wadogo nchini. 

Hayo yameelezwa leo Februari 14, 2025 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Madini Dkt.  Steven Kiruswa wakati akijibu swali la Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu aliyetaka kujua ni lini Serikali itawapatia leseni, mitambo na mitaji wachimbaji wadogo wa Singida Mashariki.

Katika majibu yake, Dkt.  Kiruswa amesema kuwa Serikali imeweka utaratibu wa kuwapatia wachimbaji wadogo maeneo ya uchimbaji kupitia maombi ya mtu mmoja mmoja yanayowasilishwa kwa Tume ya Madini. Aidha, Serikali imetenga maeneo maalum kwa wachimbaji wadogo katika Mkoa wa Singida, yakiwemo Mhintiri, Londoni, na Sambaru.

Dkt. Kiruswa amesema kuwa, STAMICO kupitia vituo vya mfano inaendelea kutoa huduma ya ukodishaji wa vifaa muhimu kama vile compressors na pampu za maji kwa gharama nafuu ili kuongeza tija katika shughuli za uchimbaji mdogo wa madini nchini.

Amesisitiza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini nchini, ikiwa ni pamoja na utoaji wa leseni, upatikanaji wa mitambo, na uwezeshaji wa kifedha ili kuboresha shughuli za uchimbaji na kuongeza tija katika sekta hiyo.

Aidha, ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata mitaji kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao, Dkt. Kiruswa amesisitiza kuwa, STAMICO imeingia makubaliano na taasisi za fedha kama CRDB, NMB, AZANIA, na KCB. Kupitia taasisi hizi, wachimbaji wadogo wanaweza kupata mikopo kwa masharti nafuu ili kuboresha shughuli zao za uchimbaji.

Naibu Waziri Dkt. Kiruswa amebainisha kuwa, kwa lengo la kuwaelimisha Wachimbaji Wadogo kuhusu fursa hizo, Wizara ya Madini kwa kushirikiana na STAMICO na Tume ya Madini imekuwa ikiendesha semina na makongamano katika mikoa mbalimbali nchini na kwamba Semina hizo zinawawezesha Wachimbaji Wadogo kuelewa taratibu za kupata maeneo, mitambo, na mikopo ili kuongeza ufanisi katika sekta ya madini.

Hatua hizo za Serikali zinadhihirisha dhamira yake ya kuhakikisha Wachimbaji Wadogo wanapata msaada unaohitajika ili kuboresha shughuli zao, kuongeza vipato vyao na kuchangia zaidi katika uchumi wa nchi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals