[Latest Updates]: Waandishi wa Habari Wanne Wapata Ajali Ziarani Kagera

Tarehe : July 3, 2020, 10:49 a.m.
left

Na Issa Mtuwa – WM Kagera

Waandishi wa Habari  Wanne Nazareth Ndekia wa TBC 1, Salma Mrisho wa Star TV, Emmanuel Ibrahim wa Clouds Tv na Victor Bariety wa Channel Ten wa kituo cha Geita wamepata ajali wakiwa kwenye Ziara ya Waziri wa Madini Doto Biteko Mkoani Kagera.

Ajali hiyo imetokea mara baada ya Dereva kuwakwepa watoto na kuacha Barabara na Kuingia mtaroni. Mara baada ya kupata ajali hiyo walikimbizwa kwenye Kituo Cha Afya Mrusagamba.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mrusagamba Benedicto Igulu alisema, majeruhi wote wanaendelea vizuri na wamepatiwa matibabu huku Nazareth Ndekia amepata maumivu kiasi ya Kichwa na Shingo na kwamba amepelekwa Kituo cha Afya Runzewe.  Salma Mrisho wa Star TV amepasuka kidevuni na kushonwa nyuzi mbili na anaendelea vizuri huku wengine wawili wamepatiwa matibabu ya kawaida na wote wameruhusiwa.

Mmoja wa Majeruhi Victor Bateiry alisema ajali hiyo ilitokana na uwepo wa watoto barabarani ambapo hawakuona msururu wa Magari ya msafara yaliyokuwepo na kwamba barabara ilikuwa na vumbi sana kiasi cha kuona gari za nyuma kuiona kirahisi.

Ziara hiyo  ilikuwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Geita na Kagera.

Waandishi wengine waliokupo kwenye ziara hiyo ni pamoja na Basir Elius wa ITV, Mariam Shabani mwakilishi wa EATV na Azam TV na George Binagi wa BMG. Waandishi walikuwa kwenye magari mawili tofauti.

Wananchi waliosaidia gari hiyo kuiondoa walisema eneo la kona hiyo kumekuwa na ajali kadhaa huku wakisema hata kwenye msafara wa mbio za mwenge siku za nyuma gari imewahi pata ajali kwenye kona hiyo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals