[Latest Updates]: Biteko kuunda Tume maalumu kuchunguza Migodi

Tarehe : June 18, 2018, 11:50 a.m.
left

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kuwa ataunda Tume Maalumu kwa ajili ya kuchunguza migodi yote nchini ikiwa ni pamoja na utambuzi wa aina ya madini yanayopatika katika migodi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro lengo likiwa ni kudhibiti utoroshaji wa madini nchini.

Baadhi ya wananchi kijijini Ipanko wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko alipokuwa katika ziara ya kikazi katika Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kukagua shughuli za utendaji wa wawekezaji wa migodi

Biteko aliyasema hayo wakati wa ziara yake mkoani Morogoro na kuongoza kuwa, madini yote yaliyopo katika ardhi ya Tanzania ni mali ya watanzania hivyo yanapaswa kuwanufaisha watanzania kwanza.

“Naombeni watanzania wote mjue kuwa madini haya ni mali ya watanzania wote hivyo tunapaswa kuyalinda na kutoa taarifa sahihi kwa serikali kama kuna mtu anaiibia serikali kwa namna moja au nyingine ili serikali iweze kuchukua hatua za kisheria dhidi yake,” aliongeza Biteko.

Pia, Biteko alipiga marufuku wawekezaji kutumia fedha zao kuwanyanyasa wananchi waliopo kwenye maeneo ambayo kuna migodi.

“Najua hawa wawekezaji wanapesa nyingi sana hivyo isiwe sababu ya kuwarubuni baadhi ya wananchi na kuwatesa wananchi wengi hususani waliopo kwenye maeneo ya madini,” alisisitiza Biteko.

Biteko alisema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli inawapenda sana kuwa na wawekezaji wengi wenye tija ambao siyo wababaishaji.

Aidha, Biteko alisema kuwa haiwekani mwekezaji akawekeza Bilioni 42 halafu akachangia madawati na mifuko ya saruji katika jamii kama ndio mchango wake, na kuongeza kuwa, wanapaswa kuchangia kulingana na kiasi ambacho wamewekeza kwa faida na manufaa ya wananchi.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi kijijini Ipanko Wilaya ya Ulanga wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Morogoro ya kukagua shughuli za uwekezaji wa migodi.

Pia, Naibu Waziri  Biteko alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Ulanga  Goodluck Mlinga kwa kuwapigania wananchi wake kwa kuzifikisha kero mahali husika na kutafutiwa ufumbuzi.

Nao, baadhi ya wananchi akiwemo Pangarasi Kanyali, Cyprian Kanyali, Micky Sengo, Doedatus Moholeli, Hilda Linoma na Fredrick Kazimoto  walimpongeza Naibu Waziri wa Madini Mhe Biteko kwa kufika kijiji hapo na kusiliza kero zao kwani wana amini zitatafutiwa ufumbuzi kwa kufuata sheria na katiba ya nchi.

“Toka sisi tuzaliwe hatujawahi kutembelewa na waziri na kusikiliza kero zetu kama ambavyo wewe umefika kijijini kwetu leo hii tunajisikia wenye amani na furaha kwa kuwa tunajua kero zetu tunazifikisha moja kwa moja kwa kwa Rais wetu kupitia wewe waziri,” walisema wananchi hao

Awali, Mbunge wa Jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga alisema kuwa lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kujionea kero wanazokumbana nazo wananchi kupitia wawekezaji wa sekta ya madini ili kuzitafutia ufumbuzi.

Imeandaliwa na;

Fredy Mgunda, Morogoro

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals