[Latest Updates]: Watendaji Wizara ya Madini Watakiwa Kupanga Mikakati Kuongeza Bajeti ya Wizara

Tarehe : Oct. 6, 2023, 9:13 a.m.
left

Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amewataka Watendaji wa Wizara na Taasisi  kujipanga  kimkakati kwa kubuni  miradi yenye tija kwenye Sekta ya Madini itakayowezesha  kuongeza Bajeti ya Wizara  na  kuhakikisha inakwenda  sambamba na Vipaumbele vya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2023/24,   Dira ya 2030 Madini ni Maisha na Utajiri pamoja na Vipaumbele vya Taifa.

Ametoa rai hiyo leo Oktoba 6, 2023, wakati wa kikao chake na baadhi ya Watendaji hao wa Wizara na Wakuu wa Taasisi za Wizara,  ambacho pia kimehusisha watendaji wanaohusika na masuala ya Mipango, Fedha na Rasilimaliwatu kilicholenga kujadili na kujipanga kutekeleza maelekezo, vipaumbele vya Wizara, majukumu, mipango na program mbalimbali ambazo zilijadiliwa wakati wa vikao vya Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde alivyofanya na taasisi zote chini ya Wizara baada ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Waziri wa Madini kwa lengo la kufahamiana, kujengeana uelewa na kuweka mikakati ili kuongeza tija kwenye Sekta ya Madini

Aidha, katika kikao hicho, watendaji hao wamepata wasaa wa  kufahamishwa kuhusu namna  ya kuandaa mipango na miradi ya kisekta yenye  tija kwa taifa  kwa kuhakikisha inakwenda sambamba na vipaumbele vilivyopangwa na Wizara na vile vya kitaifa.

Akizungumza katika kikao hicho, Mchumi Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango Khalid Shekimweli amesisitiza kuwa miradi na mipango inayopangwa na sekta ni vema ikazingatia maeneo makuu ya msingi ambayo ni pamoja na kuzingatia masuala yanayohusu huduma muhimu za kijamii, yanayokusudia kuondoa umaskini pamoja na kukuza uchumi.

Awali, Mkurugenzi wa Sera na Mipango  Wizara ya Madini Bw. Augustino Olal ameeleza kuwa katika Mwaka wa Fedha wizara imepangiwa bajeti ya Shilingi Bilioni 89.3 ambayo imelenga kutekeleza vipaumbele Sita vya Wizara na kuvitaja kuwa ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli, kuongeza  Mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa;  kuendeleza Madini Muhimu na Madini Mkakati; Kuwaendeleza na kusogezaHuduma za Ugani kwa Wachimbaji wadogo; kuhamasisha shughuli za Uongezaji thamani Madini na kuhamasisha  uwekezaji na Biashara katika sekta ya Madini na Uanzishwaji wa Minada na Maoneshi ya Madini ya  Vito.

Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals