[Latest Updates]: Serikali Yaanza Mpango wa Ununuzi wa Dhahabu

Tarehe : Sept. 24, 2023, 9:03 a.m.
left

 

•Yapanga kununua Tani 6

•TRA watoe elimu kuhusu kodi ya 2%

Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imeanza mpango maalum wa ununuzi wa Madini ya dhahabu kwa lengo la kuongeza akiba ya nchi ya fedha za kigeni.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakati akifungua Maonesho ya Sita (6) ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Dkt.Biteko aliipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kuanza mpango wa ununuzi wa Madini ya dhahabu na kuhifadhi ambapo mpaka sasa BoT imenunua kiasi cha kilogram 418 za dhahabu yenye kiwango cha asilimia 99.9. 

Akizungumza kuhusu mpango huo Dkt.Biteko alisema kuwa BoT imepanga kununua kiasi cha Tani sita kutoka kwa wachimbaji na wauzaji wa Madini nchini.

Vilevile kuhusu maendeleo ya Sekta Madini, alisema uwepo wa viwanda vizuri vyenye teknolojia ya kisasa katika uchakataji  na usafishaji wa madini ya dhahabu ndani ya nchi  kumepelekea kujenga imani kwa wanunuzi mbalimbali akiwemo  BoT tofauti na awali kabla ya kuwepo kwa viwanda uchakataji na usafishaji kufikia kiwango cha asilimia 99.9.

Akielezea juu ya mpango huo Dkt. Biteko alielekeza kuwa ni vyema kuwepo na mkakati mzuri wa kuwafiki wachimbaji wadogo popote watakapo chimba ili wauze dhahabu kwa uwazi na bei itakayoendana na soko la Dunia kukifanyika hivyo kutaondoa mawazo ya  utorosha wa Madini.

Pia ameelekeza kuundwa Kanuni mpya za uchenjuaji Madini ili wachenjuaji waweze kufanya kazi zao kwa imani na uhakika kwa kufuata hizo kanuni zitakazo undwa.

Akizungumza kuhusu Vision 2030 ni Maisha na Utajiri , Dkt. Biteko alisema kuwa mpango wa Serikali ni kuwa ifikapo 2025 sekta ya Madini ichangie asilimia 10 katika pato la taifa hivyo juhudi zifanyike katika ukusanya mapato.

Sambamba na hapo aliwaelekeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo wa Madini juu ya malipo ya asilimia mbili (2%) kwa wachimbaji wadogo katika uzalishaji wao ili wapate elimu hiyo na kuona umuhimu wa kulipa kodi husika.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals