[Latest Updates]: Kampuni 3 kuuza Tanzanite katika mnada wa Mirerani

Tarehe : July 28, 2017, 9:19 a.m.
left

Kampuni tatu za uchimbaji madini ya Tanzanite zimejitokeza kuuza madini hayo katika mnada wa tatu wa madini ya Tanzanite unaofanyika katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila( katikati) akielezwa jambo na Vikosi vya ulinzi na usalama, katika eneo linalotumika kufanyia mnada wa Madini ya Tanzanite katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.[/caption]

Mshindi wa mnada huo atatangazwa Desemba 21 katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.

Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka amezitaja kampuni hizo kuwa ni Tanzaniteone yenye ubia na Shirika la Madini Tanzania( STAMICO), Tanzanite Afrika na Classic Gems.

Akizungumzia mnada huo, Kamishna Mchwampaka alisema kuwa utaratibu  wa kufanya Mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji na wafanyabiashara wazalendo kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.

Mchwampaka alifafanua kuwa, mnunuzi atakayefanikiwa kununua madini katika mnada huo ni yule tu atakayetoa bei ya juu ambayo imefikia au kuvuka bei inayotokana na Wathamini wa Serikali (Reserve Price).

Aliweka wazi kuwa zoezi hilo linafanyika kwa njia ya uwazi ambapo wanunuzi wa ndani na nje wanapata fursa ya kutazama madini na hatimaye kupata nafasi ya kutayarisha bei zao kwa siri ambazo zitatumbukizwa kwenye sanduku la Zabuni. Aidha, viongozi wa Wizara ya Madini, Wizara ya Fedha, Viongozi wa Mkoa wa Manyara, TRA na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mkoa wa Manyara wanashirikiana kwa pamoja kuhakikisha kuwa mnada huo unafanyika kwa ufanisi.

Wanunuzi kutoka mataifa mbalimbali wakifanya uthamini wa Madini ya Tanzanite kabla ya mnada kufanyika katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.[/caption]

Aidha, mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki na kodi nyingine ikiwa ni pamoja na tozo ya Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro.

Hadi kufikia Desemba, 19,2017, zaidi ya wanunuzi 55 tayari wamejaza fomu za kuwawezesha kushindana kwenye  zabuni za kununua madini hayo,wakiwepo watanzania 39 na wanunuzi 16 kutoka nje ya Tanzania

Kamishna Mchwampaka alisema kuwa minada kama hiyo pia hufanyika kwa nchi za Afrika zenye madini ya Vito kama vile Zambia( emerald), Zimbabwe ( Almasi) pamoja na Afrika kusini ( Almasi).

Imeandaliwa na:

Zuena Msuya, Manyara

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals