[Latest Updates]: Naibu Katibu Mkuu Madini Afanya Mahojiano na Jarida Maarufu la The New Jeweller

Tarehe : Sept. 8, 2023, 4:41 p.m.
left

Mahojiano  kuhamasisha fursa za uwekezaji Sekta ya Madini Nchini 

Na Wizara ya Madini- Bangkok

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo Septemba 7, 2023 alifanya Mahojiano na Mwakilishi Maalum wa Jarida la The New Jeweller, Anand Parameswaran katika Maonesho ya 68 ya Vito na Usonara yanayoendelea jijini Bangkok nchini Thailand.

Jarida hilo ni maalum katika kuchapisha na kutangaza masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini katika nyanja zote zinazohusu mnyororo mzima wa shughuli za uongezaji thamani madini duniani hususan  bidhaa za madini ya Vito na Usonara.

Kutokana na Tanzania kuwa kivutio katika maonesho hayo ambapo inatajwa kwa sehemu kubwa madini ya vito yanayopatikana kwenye maonesho hayo yana asili ya Tanzania, uwepo wake katika maonesho hayo umekuwa kivutio kikubwa kwa wafuatiliaji wa masuala ya madini.

Aidha, kufanyika kwa mahojiano hayo kumetoa nafasi kwa Tanzania kuendelea kuhamasisha fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya madini nchini ikiwemo azma ya Serikali ya kurejesha minada ya madini nchini lengo likiwa ni kuwavutia zaidi wanunuzi na wauzaji wakubwa wa madini kutoka maeneo mbalimbali duniani kufika Tanzania.

Akizungumza na Mwakilishi huyo, pamoja na masuala mengi yaliyozungumzwa, Mbibo amemweleza mambo kadhaa ikiwemo mazingira wezeshi ya kibiashara katika Sekta ya Madini ambayo yamekuwa moja ya kichocheo kikubwa kinachopelekea wawekezaji wakubwa kuichagua Tanzania.

Pia Mbibo amemweleza kwamba, Serikali imekuwa ikizifanyia kazi kwa karibu changamoto na mapungufu ambayo yameonekana kuwa kikwazo katika biashara ya madini ambapo imewezesha kufanyika kwa marekebisho katika Sheria ya Madini na Kanuni mbalimbali zinazosimamia Sekta ya madini nchini.

Kupitia mahojiano hayo, Mbibo amewaalika wadau mbalimbali kushiriki katika Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini linalotarajiwa kufanyika Oktoba 25 na 26, 2023  jijini Dar es salaam.

Jarida la The New Jeweler hutolewa kila Mwezi na kusambazwa maeneo mbalimbali duniani.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals