[Latest Updates]: Naibu Waziri wa Madini Ashuhudia Utiaji Saini Mkataba Mnono wa Mauziano Makaa ya Mawe

Tarehe : May 10, 2022, 8:49 a.m.
left
  NAIBU WAZIRI WA MADINI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA MNONO WA MAUZIANO MAKAA YA MAWE

NAIBU Waziri wa Madini, Dkt.Steven Kiruswa ameshuhudia utiaji saini mkataba mnono kati ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Kampuni ya ABSA ambapo tani 60,000 zitauzwa kwa mwezi kwa wawekezaji hao kwa kipindi cha miaka mitano.

Hafla hiyo ya utiaji saini mkataba kati ya STAMICO na mwekezaji Kampuni ya ABSA ya nchini Uswiss imefanyika leo Mei 10, 2022 jijini Dodoma.

Dkt.Kiruswa amesema, STAMICO itakusanya mapato wastani wa shilingi bilioni 4.16 kwa mwezi sawa na wastani wa shilingi bilioni 50 kwa mwaka. 

Pia, STAMICO itatoa ajira za zisizo za moja kwa moja 600 na fursa nyingine za ajira kwa Watanzania katika mradi huo.

Amempongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt.Venance Mwasse na Menejimenti yake kwa kuwa wabunifu katika kutafuta masoko nje ya nchi. Aidha ameishukuru STAMICO kwa maamuzi ya kukubaliana na Kampuni ya ABSA katika kufanya biashara nchini.

"Ni matumaini yangu kuwa makubaliano haya yaliyosainiwa yatakuwa na manufaa kwa pande zote mbili,"amesema Dkt.Kiruswa.

Akizunguzia mafanikio ya STAMICO, Dkt.Kiruswa amesema, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi 2022, katika mradi wa Kabulo, tani 17,324 za makaa ya mawe zilichimbwa ambapo tani 12,792 zenye thamani ya shilingi 1.2 ziliuzwa na kulipa serikalini shilingi 174,191,290.87 ikiwa ni mrabaha na ada ya ukaguzi.

Dkt. Kiruswa amempongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelelea kuifungua nchi ili wawekezaji waweze kuja kuwekeza Tanzania.

"Niwahakikishie wawekezaji wetu wa makaa ya mawe kuwa Tanzania ni nchi salama, inayojali wawekezaji na inayozingatia sheria mbalimbali za nchi na kimataifa. Wizara itahakikisha pia inafuatilia mwenendo mzima wa mkataba huu ili kupata matokeo chanya kwa Shirika na Kampuni ya ABSA," amesema.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse amesema, tukio hilo ni matokeo ya mkakati wa kuanza uchimbaji mkubwa wa makaa ya mawe. (mass coal mining)

Amesema, maandalizi yamekamilika katika ukarabati wa miundombinu ya barabara, daraja na mgodi wa chini ambapo uchimbaji umeanza.

Dkt.Mwasse amesema, STAMICO imesaini mkataba mkubwa wakihistoria ambapo STAMICO itauza makaa ya mawe tani 60,000 kwa kila mwezi kwa kampuni ya ABSA.

"Mkataba huu ni wa kipindi cha miaka mitano, thamani ya mkataba huu ni dola za Marekani milioni 108 na zaidi, ya shilingi bilioni 250 za kitanzania kwa miaka hiyo mitano,"amesema Dkt.Mwasse.

Kwa upande wake Rais wa Kampuni ya ABSA, Bw.Gerges Schmickrath ameishukuru Wizara kupitia STAMICO kwa kuaminiwa kuwekeza katika mradi wa makaa ya mawe. Amesema, mradi huo utakuwa na manufaa kwa watanzania kwa kuongeza pato la Taifa.

Hafla ya utiaji saini mkataba wa mauziano wa makaa ya mawe yanayotoka katika Mkoa wa Songwe katika mgodi wa Kabulo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Madini na Shirika la Madini la Taifa.

ReplyForward

 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals