Tarehe : Oct. 1, 2018, 7:48 a.m.
Na Asteria Muhozya, Morogoro
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amewataka Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini kuhakikisha kwamba wizara hiyo haipati hoja kutokana na kukikukwa kwa taratibu za manunuzi baada ya wajumbe hao kupatiwa mafunzo kuhusu Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakikabidhi[/caption]
Pia, wajumbe hao wametakiwa kuhakikisha wanafamu kwa weledi Sheria na Kanuni za manunuzi ili waweze kutoa maamuzi sahihi.
Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Wajumbe wa Wizara hiyo yaliyofanyika katika ofisi za Madini Mkoa Morogoro tarehe 21 Septemba,2018.
Naibu Waziri Nyongo alisema hitaji la kuwapatia mafunzo wajumbe hao linafuatia upya wa wizara hiyo ikiwemo wajumbe wa bodi hiyo ambao wengine wametoka katika sekta mbalimbali hivyo mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuzingatia sheria na kanuni za manunuzi zilizoanishwa.
“Masuala ya manunuzi yanalalamikiwa sana kutokana na ucheleweshaji wa maamuzi. Lakini pia, manunuzi ya umma yamekuwa na matatizo kutokana na kuwepo Mikataba mibovu kwa hiyo baada ya ninyi kupatiwa mafunzo haya, sitarajii vitu kama hivi kujitokeza.
Pia, Naibu Waziri Nyongo aliwataka wajumbe wa bodi kuhakikisha kuwa, mafunzo waliyoyapata yanawasaidia kuepukana na vitendo vya rushwa wakati wa kusimamia shughuli za manunuzi ya wizara.
“Ukiiba mali ya umma kuna siku wengine watakuja na watahoji. Siku zote mali ya umma ni ya kuogopa,” alisisitiza Naibu Waziri nyongo.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakiwa wakijadiliana wakati wa mafunzo kuhusu masuala ya manunuzi kwa wizara hiyo[/caption]
Naye, Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Wizara ya Madini, Issa Nchasi, alisema kuwa, wakati wa mafunzo wajumbe hao walipata nafasi ya kujifunza kuhusu Sheria, Mikataba na Kanuni za Manunuzi ikiwemo kupata uzoefu wa shughuli za manunuzi na namna zinavyofanyika.
Akizungumzia manufaa ya mafunzo, Nchasi alisema kuwa yamekuwa na manufaa makubwa kwa kuwa yatawawezesha wajumbe kutoa maamuzi sahihi ikiwemo kumshauri Afisa Masuhuli kufuata Sheria na Kanuni ili kuepuka ununuzi ambao hauzingatii sheria.
Aliongeza kuwa, mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha wajumbe kuelewa Sheria ili kufanya kazi zao kwa weledi.
Kwa upande wake, Mkufunzi kutoka Wataalam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Paschal Komba aliipongeza wizara ya Madini kwa kutoa mafunzo hayo kwa wajumbe wa bodi hiyo na kuelea kuwa, yatawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria na taratibu za ununuzi wa umma.
Mafunzo hayo yalitolewa na Wataalam kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA).
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.