[Latest Updates]: Wizara ya Madini, Ubalozi China Waendeleza Majadiliano ya Utafiti wa Kina

Tarehe : March 3, 2025, 2:16 p.m.
left

Ni mwendelezo wa Majadiliano yaliyoanzishwa na Makamu wa Rais kuhusu Utafiti wa Madini

Wajadili  uendelezaji Madini Mkakati, Teknolojia na Kuendeleza Wataalam

 
Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amekutana na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Mhe. Chen Mingjian katika kikao kilicholenga kujadili fursa na maeneo mbalimbali ya ushirikiano katika Sekta ya Madini ikiwa ni mwendelezo wa  mazungumzo kati ya  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip  Mpango na kiongozi huyo .

Katika mazungumzo yao, Dkt. Mpango aliiomba Serikali ya China  kupitia balozi huyo kusaidia shughuli za utafiti wa madini Tanzania, ambapo baada ya mazungumzo yao,  Serikali ya China imetuma wataalam wawili kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti  ya nchini humo ili kufuatilia na kujua mahitaji ya utafiti na maeneo mengine ya mashirikiano kati ya Tanzania na China
                                   
‘’Kikao nilichokiongoza leo Machi 3, 2025,  kimejadili maeneo ya ushirikiano, na sisi kwa upande wetu tumeweza kubaini maeneo matatu muhimu ambayo Serikali ya china inaweza kutusaidia  katika shughuli za utafiti na kujenga uwezo wa watumishi wa Wizara  kulingana na mahitaji,’’ amesema Dkt. Kiruswa.

Maeneo matatu ambayo wataalam wa Wizara wakiongozwa na Dkt. Kiruswa waliyoweza kuyabaini ni pamoja na  kusaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina wa jiofizikia (high resolution airborne geophysical survey) hususani kwa kuanzia eneo la Mkoa wa Dodoma;

Maeneo mengine ni pamoja na kusaidia upatikanaji wa fursa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wataalam  wa ndani  katika maeneo ya teknolojia za kisasa kama vile ukusanyaji na uchakataji wa taarifa za jiosayansi; na kusaidia kuleta teknolojia za kisasa za utafiti na uchakataji wa taarifa za utafiti wa madini ikiwa ni pamoja na matumizi ya ndege nyuki katika utafiti wa madini nchini.

Wengine walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman  Mwanga Kamishna, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jilojia na Utafiti wa Madini Tanzania, (GST) Dkt. Mussa Budeba, Mkurugenzi wa Huduma za Jiolojia (GST) Dkt. Ronald Massawe, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Makamba, Makamba na maafisa kutoka ubalozi wa China nchini Bw. Chu Kun na wataalm kutoka Taasisi ya Jiolojia China Bw. Ren Junping na Bw. Sun Kai.


# Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri

# Invest In TanzaniaMiningSector

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals