[Latest News]: Tanzania Kuwa kitovu cha Biashara ya Madini: Waziri Biteko

Tarehe : July 23, 2022, 10:26 p.m.
left

SERIKALI imepanga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara ya madini kwa kuvutia wawekezaji wengi duniani kuja kuwekeza katika sekta  hiyo na kufungua fursa nyingi za kuchimba madini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Madini, Dkt.Doto Biteko alipokutana na kuzungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika mkutano uliolenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za uchimbaji  Julai 20, 2022 mkoani Kigoma.

Dkt. Biteko amesema, mataifa mengi yanakuja nchini kujifunza kuhusu usimamizi wa Sekta ya Madini na hasa sekta ndogo ya wachimbaji wadogo na hivyo kuifanya Tanzania kuwa mfano kwa mataifa.

Amesema Serikali imeendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa wachimbaji katika Sekta ya Madini kuweza kuwekeza katika uchimbaji wa madini na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara hiyo.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema wachimbaji wadogo wapo kwenye moyo wake, tena anawaita wachimbaji wangu wadogo, anawapenda na kuwathamini sana, anatamani kuona changamoto walizonazo wachimbaji hao kote nchini zinamalizwa kwa haraka," amesema.

Akizungumzia mikopo kwa wachimbaji wa madini, Dkt.Biteko amesema Serikali imefanya kazi kubwa kuzungumza na taasisi za fedha ili zianze kukopesha wachimbaji wadogo na tayari zipo baadhi ya taasisi zinazotoa mikopo kwa wachimbaji.

Dkt. Biteko ameongeza kuwa, Sekta ya Madini ina wajibu wa kutoa ajira kwa Watanzania, kukuza uchumi wa nchi na kujenga utajiri na kuwaondolea umaskini watu.

Amesema, changamoto ya soko kuu la madini la mkoa linaloendelea kujengwa Serikali itakamilisha ujenzi wa soko ili watu wengi waweze kuleta madini yao kuuza madini yao hususan wafanyabiashara kutoka nchi za jirani.

"Serikali itaendelea kufanya utafiti kwenye maeneo yanapochimbwa madini nchini ili wachimbe na kupata manufaa,"ameongeza. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe.Thobias Andengenye amewapongeza wachimbaji wa mkoa wa huo kwa kufanya kazi na kuendelea kuutangaza mkoa kwa uchimbaji madini katika maeneo mbalimbali.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals