[Latest Updates]: Waziri Mavunde Aagiza Kurekebishwa kwa Maduara na Miamba Inayoning'inia Eneo la Uchimbaji Mwakitolyo Shinyanga

Tarehe : Nov. 11, 2023, 7:54 p.m.
left

 

Kufuatia Taarifa ya ukaguzi uliofanywa na timu ya wataalamu iliyoundwa na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde kuhusu  uchambuzi wa mikataba kati ya Vikundi vya wachimbaji wadogo wa madini  na wabia(technical support) kwenye  leseni za uchimbaji mdogo  zilizopo katika eneo la Mwakitolyo  mkoani Shinyanga  kamati imebaini sehemu kubwa ya maduara hayapo katika hali salama  ya uchimbaji.

Akiwasilisha taarifa hiyo,Mwenyekiti wa Timu ya watalaamu Mhandisi Ally Samaje amebainisha kwamba eneo la uchimbaji la mwakitolyo linahitajika kukatwa kwa miamba inayoyoning’inia na kurekekebisha maduara ili wachimbaji wachimbe kwa usalama zaidi na kuongeza uzalishaji kuliko ilivyo hivi sasa.

Sambamba na hapo kamati imebaini kuwa uchimbaji wa pamoja (co-existence) kati ya Wachimbaji wadogo na wabia kupitia muongozo wa uchimbaji utakaosimamiwa na Wizara ya Madini.

Akipokea taarifa hiyo,Waziri Mavunde amemuelekeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Ndg. Msafiri Mbibo kuhakikisha anasimamia kwa ukaribu urekebishaji wa maduara na maeneo yenye miamba inayoning’inia kwa usalama wa wachimbaji wadogo na kuongeza uzalishaji wa madini.

“Suala la usalama katika maeneo ya uchimbaji ni suala muhimu ambalo lazima tulipe uzito mkubwa.

 

Naelekeza kwamba katika maeneo yote hapo Mwakitolyo yaliyo chini ya ubia wa msaada wa kiufundi(technical support) yarekebishwe dosari zote za kiusalama ili kuwaruhusu wachimbaji wadogo wafanye shughuli za uchimbaji katika mazingira ambayo ni rafiki.

Nataka pia niwahakikishie kwamba Hakuna mchimbaji mdogo yoyote atakayeondolewa katika eneo lake kwakuwa eneo hili liligawiwa kwa wachimbaji wadogo kama wanufaika wa kwanza.

Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuelekeza kuhakikisha tunawasimamia na kuwaendeleza wachimbaji wadogo kwa kuwapatia maeneo ya uchimbaji na pia katika upatikanaji wa mikopo na mitaji ili kuongeza tija katika shughuli zenu”Alisema Mavunde

Mkutano huo wa kupokea taarifa ulihudhuriwa na Viongozi wa Mkoa wa Shinyanga,Kamati za Ulinzi na Usalama  pamoja na wachimbaji wa eneo la Mwakitolyo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals