Tarehe : April 28, 2018, 12:06 p.m.
Naibu waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema kuwa Wizara yake haitatoa leseni ya uchimbaji madini kwa mwekezaji aliyepewa leseni ya kuchimba madini katika eneo la kijiji cha Ishokelahela wilaya ya Misungwi baada ya kushindwa kuendeleza eneo hilo kama Sheria ya Madini inavyoelekeza.
Akiwa katika ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wilayani humo, Nyongo alisema kuwa mwekezaji huyo alipewa leseni ya uchimbaji wa madini kwa kipindi cha miaka 10 na hakuna uendelezaji wowote alioufanya katika machimbo hayo.
Uamuzi huo umetokana na malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho wakati wakitoa dukuduku zao kwa Waziri Mkuu kuwa, mwekezaji huyo amekuwa akiwazuia wachimbaji wadogo kuchimba madini katika machimbo hayo hali iliyopelekea Waziri Mkuu kumtaka Naibu Waziri wa Madini kulitolea ufafanuzi suala hilo.
Akitoa ufafanuzi kuhusu mwekezaji huyo, Nyongo alisema kuwa kutokana na kutoendeleza machimbo hayo mwekezaji huyo amekuwa haelewani na jamii inayozunguka machimbo hayo na kwamba hapo awali wananchi walikuwa wanafanya shughuli za uchimbaji katika katika eneo hilo kabla ya kupewa mwekezaji huyo.
‘’Mwekezaji huyu anayefahamika kwa jina la Badir Soud kwa kuwa leseni yake imeisha na ameomba tena leseni hiyo ya uchimbaji hatutampa, na sisi kama Wizara ya Madini tutawapatia wananchi wachimbe wakiwa katika mfumo wa vikundi’’ alisema Nyongo.
Aliendelea kueleza kuwa, pamoja na kutokuendeleza mgodi huo katika kipindi hicho, mwekezaji huyo hajapeleka vifaa kwa ajili ya shughuli za uchimbaji katika eneo la mgodi jambo ambalo linaikosesha Serikali mapato.
Naibu Waziri Nyongo alitumia fursa hiyo kuwaagiza wachimbaji wa madini nchini kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria za uchimbaji madini ili waweze kutambulika rasmi na kuweza kulipa kodi serikalini.
Na Mwandidhi Wetu Misungwi
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.