[Latest Updates]: Yaliyojiri Wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Madini na Uwekezaji Tanzania 2024, Uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Leo Novemba 19, 2024 Jijini Dar Es Salaam

Tarehe : Nov. 19, 2024, 12:45 p.m.
left

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

# Malengo mahususi ya mkutano huu ni kuvutia uwekezaji kutoka nje kuja nchini; kubadilishana maarifa na uzoefu mlionao katika Sekta ya Madini; kukuza usimamizi bora wa rasilimali tulizonazo za madini; kuongeza fursa za ajira na maendeleo ya jamii inayozunguka maeneo ya uchimbaji madini; kuimarisha ushirikiano kati ya serikali za nchi mbalimbali, sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo katika tasnia ya madini.

# Lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inaendelea kuongeza mchango wake, na hasa katika ukuaji wa uchumi wa nchi, kwa kuhakikisha kwamba sekta hii inachangia zaidi ya asilimia 10 katika Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025.

# Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umekua, na kukua huku ni kutokana na ongezeko la asilimia 7.3 kwa mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 9. Ni matumaini yangu kuwa ifikapo mwaka 2025 Sekta ya Madini itafikia lengo la mchango la asilimia 10 ya Pato la Ndani la Taifa.

# Kwa kuzingatia umuhimu wa sekta hii serikali imechukua hatua muhimu ya kuhakikisha kwamba wawekezaji wakubwa na wadogo kwenye Sekta ya Madini wanaendesha shughuli zao kwa tija kwa  kuwezesha mazingira wezeshi ya uwekezaji na upatikanaji teknolojia unaimarika, hii ni pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ambayo serikali imeamua kuimarisha kwa lengo la kuvutia uwekezaji na kuwezesha uwekezaji huo kuleta faida kwa kila mwekezaji.

# Kuongeza uwezo wa nishati ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, kuimarisha njia za usafirishaji kama vile barabara, reli, bandari na anga kwa kuongeza ndege na kujenga viwanja zaidi, yote haya ni kutaka kusaidia shughuli za uwekezaji kwenye Sekta ya Madini kuweza kufanyika kwa tija lakini kuwapunguzia gharama wawekezaji.

# Serikali imesogeza huduma za masoko kila mkoa, na vituo vya kununulia madini katika maeneo ambayo madini yanachimbwa, na sasa tuna masoko 44 katika mikoa mbalimbali nchini na vituo 103 vya kununulia madini hapa nchini.

# Kupitia masoko na vituo hivyo kumekuwepo na mzunguko mzuri wa ukusanyaji madini hasa katika mwaka 2023/24, ambapo madini yenye thamani ya shilingi trilioni 2.59 yaliuzwa kupitia masoko ya madini na kuiwezesha Serikali kukusanya Shilingi Bilioni 180.

# Serikali imeanzisha ziara za kimafunzo kwa wachimbaji wadogo ikishirikiana na Shirikisho la Vyama vya Wachimba Madini Tanzania (FEMATA), mwaka 2023 wachimbaji wadogo 95 walitembelea nchini China kujifunza teknolojia ya kisasa ya kutafuta masoko ya madini.

Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde

# Natoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali Tanzania kuwa sehemu ya waandaaji wa mkutano huu na kutupa kibali cha kuandaa mkutano huu.

# Naomba nitoe pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye Serikali ya Awamu Sita imeonesha dhamira ya dhati ya kuikuza sekta ya madini hapa nchini Tanzania.

# Bajeti ya Wizara ya Madini imeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 89 mpaka Shilingi Bilioni 231. Aidha, fedha hizo kwa kiwango kikubwa zimeelekezwa kwenye taasisi yetu ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST), ambapo tutakwenda kujenga maabara kubwa ya kisasa mkoani Dodoma, mkoa wa kimadini Geita na mkoa wa kimadini wa Chunya.

# Tumetenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa Helicopta ambayo itasaidia katika kufanya utafiti wa kina. Nchi yetu ya Tanzania tumefanya utafiti wa kina kwa asilimia 16 tu, ambapo Tanzania ina ukubwa Kilomita za Mraba 945,000  sawasawa na Ekari Milioni 233. Tumejiwekea malengo kwamba, ifikapo mwaka 2030 tuwe tumefika eneo lenye ukubwa wa asilimia 50 ya nchi yetu ya Tanzania.

# Katika asilimia 16 iliyofanyiwa utafiti, manufaa yafuatayo yamepatikana; Katika mwaka wa fedha 2022/23 sekta ya madini ndio ilikuwa sekta kiongozi kwa kuingizia nchi yetu fedha za kigeni, ambapo mauzo ya bidhaa nje ya nchi yalikuwa ni Dola Bilioni 3.1 sawasawa na asilimia 56 ya fedha yote ya kigeni iliyopatikana hapa nchini.

# Sekta ya Madini inaendelea kukua mwaka hadi mwaka, ukuaji wa Sekta ya Madini kwa mwaka 2021 ilikuwa ni asilimia 9.3, hivi sasa ukuaji wa Sekta ya Madini umeongezeka kufikia asilimia 11.3. Mwaka 2021 Sekta ya Madini ilichangia katika Pato la Taifa kwa asilimia 7.2, hivi sasa Sekta ya Madini inachangia kwenye Pato la Taifa kwa asilimia 9.0

# Katika mwaka huu wa fedha 2024/25, kwa siku 135 za mwaka huu wa fedha, sekta ya madini imeshaingiza katika Mfuko Mkuu wa Serikali Shilingi Bilioni 392, lengo letu ni kuingiza Shilingi Trilioni Moja ifikapo mwakani mwezi wa Sita.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals