Tarehe : Oct. 27, 2018, 8:34 a.m.
Na Asteria Muhozya,
Wizara ya Madini imeanza kukutana na Kamati Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuanzia leo tarehe 29 Oktoba hadi Novemba 1, 2018.
Katika kikao cha leo Wizara imewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Akiwasilisha Taarifa kuhusu Ujenzi wa Mgodi wa Mfano wa Lwamgasa, Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal amesema hadi kufikia mwezi Septemba,2018, kazi ya ujenzi wa mgodi na usimikaji wa mitambo ya uchenjuaji imekamilika kwa asilimia 80.
Kuhusu mradi wa One Stop Center, eneo la Mirerani, amesema uko kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi na kuongeza kuwa, jengo hilo litakapokamilika litakuwa na miundombinu mbalimbali ikiwemo huduma za Utoaji na Usimamizi wa Leseni za Madini, Uhifadhi wa madini kwa usalama , Kodi na tozo mbalimbali ikiwemo ofisi za TRA, Huduma za kifedha, ikiwemo Benki na Ofisi za Benki kuu, Huduma za tathmini na uthamini madini, Ofisi za Madini na Chumba maalum cha kufanyia minada ya madini.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.